ETI NI KWELI KUWA WANAWAKE WAREMBO HAWAOLEWI?
Sababu kubwa ni kwamba eti kuoa mwanamke mzuri sana kwa viwango vyote inaletea presha, kwa sababu atakuwa akitamaniwa na kila mwanaume, na mara nyingi kama mume atakua ni mtu wa kipato kidogo, ni rahisi mkewe huyo kuingia katika vishawisi na kutoka nje ya ndoa kwa sababu atakuwa akiwindwa na wanaume wakware.
Wengi hubainisha kuwa jambo hilo limefanyiwa utafiti na kupata ukweli wa kutosha kuwa wanaume wengi waliooa wanawake wazuri kupindukia aidha walifarki kwa maradhi ya moyo wakiwa bado na umri mdogo au wamepata maradhi ya kudumu kama vile presha na kisukari kutokana na hofu ya kuporwa wake zao hao au hata ukimwi.
Hata wale walioachwa na wake zao baada ya kushawaishiwa na wanaume wenye pesa, wengi waliishia kujinyonga au kujiua kwa kunywa sumu, na wengine waliishia kuwa watumiaji wa aidha madawa ya kulevya au matumizi ya pombe kupindukia.
Je jambo hili lina ukweli wowote?
No comments
+255716829257