Habari mpya

CHANZO, ATHARI NA TIBA ASILIA YA SARATANI YA NGOZI.

Image result for CHANZO, ATHARI NA TIBA ASILI YA SARATANI YA NGOZI.
Saratani si tu kwamba ni ugonjwa hatari lakini pia ni ugonjwa unaompa mwanadamu mateso makali kutokana na maumivu anayoyapata.
Maumivu hayo huyapata mgonjwa bila kujali kama anaugua saratani ya ngozi, ya mifupa, damu, tumbo au ya kizazi. Shida ya maradhi haya ni kwamba matibabu yake yanahitaji gharama kubwa mno.
Melanoma ni saratani ya hatari sana kwa maisha ya mwanadamu inapotokea mtu akaipata, basi maisha yake yanakuwa hatarini. Saratani hii si rahisi kuigundua ukilinganisha na saratani nyingine za ngozi lakini pia husambaa haraka zaidi mwilini kuliko saratani nyingine za ngozi.
Melanoma huweza kusambaa na kushambulia viungo vingine zaidi ya ngozi kama mifupa na ubongo. Inapofikia hatua hii saratani hii inakuwa ngumu sana kutibika.
Dalili
Dalili za saratani hii zipo nyingi na ni vema kila mtu afahamu, mojawapo ni kubadilika kwa ukubwa, rangi au ule muundo wa alama ya ngozi ambayo mtu amekuwa nayo kwa muda mrefu au umezaliwa nayo. Alama hii ni ile ambayo ina rangi nyeusi zaidi ukilinganisha na maeneo mengine ya ngozi.
Mabadiliko haya si lazima yawe yanatokea haraka haraka yanaweza kuwa yanatokea taratibu, hivyo kila mwenye baka anatakiwa kujichunguza ili kuona kama kuna mabadiliko kwenye alama hiyo ya ngozi.
Ni muhimu sana kutambua mabadiliko haya. Mabadiliko mengine ni kama yafuatayo, alama hii inaweza kuwa inavimba, kingo zake zinapoteza mzingo wake wa kawaida, alama inakua zaidi kwa eneo kwa mfano kutoka mzingo wa 4 mm na kuwa kubwa na kuzidi 6 mm.
Dalili nyingine ni alama kuanza kuwasha na kama mgonjwa atachelewa kugundua tatizo basi zitajitokeza alama kwenye ngozi ambayo itapasuka na kuwa kidonda.
Alama hiyo baadaye inaweza ikawa inatoa damu na kuwa na maumivu. Kama matibabu hayatafanyika basi saratani hii husambaa na dalili zifuatazo huweza kuonekana :
Tezi za mwili za kwenye makwapa na kwenye nyonga huvimba, mgonjwa atatokwa na uvimbe kwenye ngozi, atapoteza uzito kwa kasi bila kujua sababu, atapata kikohozi kisichoisha, atapoteza fahamu au kupata kifafa, ataumwa kichwa kuuma.
Tiba
Kuna tiba nyingi za kitabibu, zilizogawanyika katika makundi mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila kutumia gharama kubwa.
Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto ambayo yanatibu magonjwa mengi ikiwemo figo, kutoa sumu mwilini, kuyeyusha mafuta tumboni, kurahisisha mzunguko wa damu, kuondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.
Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku mtu anywe glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia jasho au mkojo.
Wadau wa afya wanasema kuwa ni vyema pia kunywa maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.
Maji yanarahisisha uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini, hivyo kutokana na umuhimu huo ni vyema kunywa maji ya moto yatakayofanya kazi haraka na kwa ufanisi mkubwa bila kuchosha figo.
Faida nyingine ya kunywa maji ya moto kuwa ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisaidia figo kufanya kazi kikamilifu, tofauti na maji baridi ambayo yanagandisha na kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja.
Ushauri
Unashauriwa kunywa maji moto kabla ya kufanya mazoezi kwani huko ni kujiandaa kwa ajili ya kuchuja jasho ambalo litatoa sumu. Maji ya moto yakifika tumboni yanaanza kufanya kazi moja kwa moja, kuliko yakiwa ya baridi yanaweza kusumbua kwa kuwa ni lazima yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.
Unywaji wa maji ya moto kabla ya mazoezi ni mzuri kwani mtu anakuwa kama amekula chakula. Kunywa maji ya baridi bila kuweka kitu tumboni na kwenda kufanya mazoezi
kunaweza kusababisha tumbo kuuma au maji kucheza wakati wa kukimbia kama unafanya mazoezi ya kukimbia. Lakini yakiwa ya moto ni kama umekunywa chai au kula chakula cha kawaida.
Maji ya moto ni mazuri hata kwa kupata choo, kwa vile kinarahisisha uyeyushaji na uchambuaji wa kinachotakiwa na kisichotakiwa, wanaokunywa ya baridi wana uwezekanao mkubwa wa kupata haja kubwa kwa shida.
Ni vyema kunywa maji moto yaliyochemshwa na kuyaacha yapoe na kuwa vuguvugu na kuongeza limao na asali mbali na kuongeza ladha, asali na limao vina faida kiafya.
Kunywa maji ya uvuguvugu au ya moto ni vyema kwa kuwa hufanya kazi moja kwa moja kutokana na hali ya tumbo kuwa na joto muda wote.
Maji ni muhimu kwa mwili wako, yakiwa ya moto ni bora zaidi, kwa kuwa yanatoa rangi ya njano ya mkojo na kuufanya uwe msafi na wenye rangi angavu.
Ushauri ni kuwa ukiwa na alama yoyote mwilini inayokuwa kamuone daktari haraka.
Tiba
Tengeneza juisi ya kitunguu maji.Changanya na maziwa ya unga na unga wa kibiriti upele as-far robo ya kijiko cha chai(1.25ml).Changanya pamoja mpaka iwe krimu.
Pakaa sehemu yenye matatizo kutwa mara moja (1×1).Baada ya kuoga jioni pakaa na mafuta ya zaituni

No comments

+255716829257