Habari mpya

KOREA KUSINI: MAANDAMANO YAENDELEA KUMPINGA RAIS WA NCHI HIYO..

 Maandamano mjini Seoul
Kwa wikendi ya tatu mfululizo wananchi wa Korea Kusini waliyojawa na ghadhabu wameamua kumiminika katika barabara za mji mkuu wa Seoul kumtaka rais wa taifa hilo Park Guen Hye kujiuzulu.
Mandamano ya leo yanatarajiwa kuwa makubwa zaidi. Viongozi wa maandamano hayo wanasema mamilioni ya watu watashiriki.
Maelfu ya maafisa wa polisi wa kukabiliana na ghasia,wamepelekwa katika mji mkuu wa Seoul kukabiliana na waandamanaji hao wanaopinga serikali kufika ikulu ya rais.
Rais Park Guen Hye, anatuhumiwa kwa kuwa na uhusiano wa karibu na Choi Soon-sil, anayekabiliwa na shtaka la kujaribu kuibia serikali fedha nyingi kupitia kampuni kadhaa za taifa hilo.
Bi Choi amekamatwa na kushtakiwa kwa ubadhirifu wa pesa za umma na utumizi mbaya wa mamlaka.
Maafisa kadhaa wanaohudumu katika ofisi ya Rais Guen Hye pia wanachunguzwa dhidi ya sakata hiyo.

No comments

+255716829257