Simba
Mchezo wa pili wa Simba wa Ligi Kuu ya Vodacoma (VPL) kwa msimu wa 2016/2017 umepigwa katika uwanja wa taifa dhidi ya JKT Ruvu na mchezo huo ukimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Simba itabaki ikijilaumu kwani kuanzia dakika ya 60 ilikuwa ikilishambuliaji kwa kasi lango la JKT Ruvu lakini ilishindwa kutumia ipasavyo nafasi ilizokuwa ikizipata na hivyo kuambulia nafasi moja ya mchezo huo.
Baada ya mchezo huo, Simba sasa imefikisha alama nne na mchezo unaofuata inataraji kucheza na Ruvu Shooting.
Matokeo ya michezo mingine ni;
Azam 3 – 0 Majimaji
Mbao 0 – 1 Mwadui
Mtibwa Sugar 2 – 1 Ndanda.
CHANZO: Dewj blog