RC Paul Makonda Aitwa Tume ya Haki za Binadamu Kujieleza
Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesikitishwa na matamshi
ya Mhe. Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam yanayokiuka misingi
ya utawala bora aliyoyatoa tarehe 25 Agosti, 2016 wakati wa kuaga miili
ya askari Polisi watatu waliouawa Mbande, Mkoani Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume, Mhe.
Bahame Tom Nyanduga, leo (Agosti 26, 2016) Mhe. Makonda ametumiwa barua
ya wito inayomtaka afike makao makuu ya Tume mtaa wa Luthuli, tarehe 30
Agosti, 2016 ili kujadili kile Tume ilichokiona kuwa ni kejeli kwa Tume
pamoja na jumuiya yote ya watetezi wa haki za binadamu.
Aidha, Tume imeona kuwa maagizo
aliyoyatoa Mkuu huyo wa Mkoa kwa Jeshi la Polisi hayana msingi wa
kisheria na hayako ndani ya mamlaka ya Mkuu wa Mkoa.
Kwa mujibu wa Kifungu cha 6(1)(f) na
(i) pia Kifungu cha 27(1) na (2) (a) vya Sheria ya Tume ya Haki za
Binadamu na Utawala Bora Sura Na. 391 ya Sheria za Tanzania 2002, THBUB
ina mamlaka ya kuchunguza mwenendo wa mtu au taasisi yoyote kuhusiana na
utendaji wa kazi zake zinapokiuka mipaka ya madaraka yake, ili kuchukua
hatua za kurekebisha ukiukwaji huo.
Imetolewa na:
(SIGNED)
Idara ya Elimu kwa Umma na Mafunzo
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA
Agosti 26, 2016
No comments
+255716829257