HII HAPA HISTORIA FUPI YA RAPPER FID Q KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA LEO AUGUST 13..
Leo agost 13, 2016 ni siku aliyozaliwa gwiji wa muziki wa Hip hop
Tanzania na Africa mashariki kwa ujumla, Farid Kubanda kutoka rock city Mwanza.
Ikiwa huyu ni nguzo na hazina kubwa ya watanzania hasa katika tasnia ya muziki
blogu hii haina budi kukupatia historia fupi ya legendary huyu.
Farid Kubanda amezaliwa tar. 13 Agosti
1982, katika
hospitali ya Bugando
iliyopo jijini Mwanza,
huyu ni msanii wa hip hop na Bongo Flava kutoka nchini Tanzania.
Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Fid Q.
Fid Q alianza shughuli za muziki mnamo miaka ya
1990. Fid Q alitoa kibao chake cha kwanza mwaka 2000 kiitwacho 'Huyu na Yule'
ambacho hicho aliimba na msanii Mr Paul. Kibao hiki kilimpa heshima kubwa,
kibao hicho kilirekodiwa katika studio za MJ records chini ya
usimamizi wake Master Jay mwenyewe.
Kibao chake cha pili kutoka kiliitwa 'Binti Malkia'
ambacho alimshirikisha Noorelly. Ilivyofika mnamo mwaka wa 2004 Fid Q alivunja
ukimya wake kwa kibao chake mahili kilichokwenda kwa jina la "Fid Q.com", na kibao hicho alikifanya
katika studio ya Baucha Records baada ya
kuhama kwa MJ.
Kibao hicho kiliirudisha ile hiphop ya Tanzania
katika ramani yake halisi na inasemekana hivyo kwasababu kipindi hicho ni kile
ambacho wasaanii wengi wa muziki wa kufokafoka walikuwa wamejiingiza katika
masuala ya uimbaji kwasababu kulikuwa na uvumi wa kwamba hip hop haikubaliki
kwa watu wa Tanzania. .Fid anatajwa kuwa Ni miongoni mwa wasanii walioleta
heshima ya hip hop Tanzania na Afrika mashariki na kibao chake kinachojulikana
kama Mwanzamwanza kilifanya vizuri ambapo ndani yake kuna uandishi wa kipekee
ambao umeenda tofauti na ule uliokuwa umezoeleka
Ilipofika mwezi wa Januri ya 26 katika mwaka wa 2008,
Fid Q alipakua kibao kiitwacho "Ni Hayo Tu"
alichomshirikisha Prof. J na hayati Langa. Kibao hicho kilibahatika
kujinyakulia Tuzo ya Kili kikiwa kama kibao bora cha muziki
wa hip hop kwa mwaka wa 2007-2008.
Fid Q ana albamu mbili kwenye soko la muziki.
Albamu ya kwanza inaitwa inayoitwa "Vina Mwanzo Kati na Mwisho".
Mwishoni mwa mwaka 2009 alitoa albamu ya pili "PROPAGANDA", ambayo
imepokelewa vizuri sana Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki.
Mashabiki wa Hip Hop wanaichukulia PROPAGANDA kama ni albamu bora kabisa, yaani
'classic'. Hivi karibuni anategemea kutoa albamu yake ya tatu itakayokwenda kwa
jina la "KitaaOLOJIA".
Leo august 13, 2016 katika kusherehekea siku ya
kuzaliwa Fid Q a.k.a Ngosha the don amewabless mashabiki wake na mzigo mkali
unaokwenda kwa jina la “SUMU”, fuata link hapa chini kusikiliza na kupakua..
DOWNLOAD
No comments
+255716829257