Habari mpya

YANAYOJIRI KATIKA ZIARA YA NETANYAHU NCHINI UGANDA..

 
 Ndege ya waziri Netanyahu
Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ametua nchini Uganda katika ziara ya kwanza kabisa kwa kiongozi wa taifa hilo la kiyahudi kuzuru Afrika tangu mwaka wa 1987.
 
 Netanyahu anakutana na viongozi wa mataifa 6 ya Afrika
Ziara hiyo ya siku 5 imeanzia Uganda, na kisha waziri Netanyahu anatarajiwa kuzuru Kenya, Rwanda na kisha Ethiopia.
 
 Usalama uliimarishwa
Ilikuwa kihoja kwa wageni waalikwa kuingia kwenye uwanja huo wa ndege kwani usalama uliimarishwa huku maafisa wa usalama wa Israeli wakishika doria na mbwa na walenga shabaha, mbali na upekuzi wa kawaida wa maafisa wa usalama wa Uganda.
Bw Netanyahu ameandamana na mkewe Sarah na ujumbe wa wafanyibiashara wa sekta mbalimbali za uchumi wa Israe.
 
Netanyahu alipata fursa ya kuhudhuria misa ya ukumbusho wa kakake Yoni mmoja wa makomando wa Irsaeli waliokufa katika shambulizi hilo.
\ Alipotua katika uwanja huo wa ndege wa Entebbe eneo kulikotokea operesheni ya kipekee miaka 40 iliyopita, ya kuwanusuru mateka wayahudi waliokuwa wametekwa na wanamgambo wa kipalestina, Netanyahu alipata fursa ya kuhudhuria misa ya ukumbusho wa kakake Yoni mmoja wa makomando wa Irsaeli waliokufa katika shambulizi hilo.
 
 Mwenge wa ukumbusho uliashwa
Ndege iliyokuwa imewabeba wayahudi hao ilikuwa imetoka Israeli ikielekea Ufaransa.
Kabla ya hapo alikagua gwaride la heshima lililoandamana na makombora 19 kwa heshma yake.
Waziri Netanyahu anasema kuwa ziara hii inalenga kuimarisha uhusiano wa taifa hilo la kiyahudi na mataifa ya Afrika ambayo Israeli inatumai kuwavutia iliwasiwaunge mkono wanaharakati wa Palestina.
 
 Baadhi ya mateka wa Entebbe walihudhuria ukumbusho huu
Mwenyeji wake rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amewakaribisha marais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Paul Kagame wa Rwanda Salva Kiir Mayardit, wa Jamuhuri changa zaidi duniani ya Sudan Kusini Edgar Lungu wa Zambia, rais wa Malawi waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, na waziri wa maswala ya Kigeni wa Tanzania Augustine Mahiga katika kikao cha faragha kinachotarajiwa kujadili maswala ya ugaidi na Usalama wa taifa ambayo Israeli imeahidi kuyasaidia kukabiliana nayo.
 
 Ndege aina ya Herculean iliyotumika katika operesheni hiyo
Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, makomando wa Israeli wameshika doria kote mjini Kampala atakozuru Waziri Netanyahu.
Israeli haijakuwa na uhusiano mwema na mataifa ya Afrika ambayo yaliiona kuwa saliti kwa kushirikiana na serikali dhalimu ya Afrika Kusini iliyokuwa ikiwatesa waafrika weusi.

 Eneo la mawasiliano lililoharibiwa katika makabiliano hayo ya Entebbe raid
Aidha mataifa ya Afrika yaliunga mkono jitihada za Uhuru wa wapalestina ambao wanakaliwa kimabavu na Isreali na hivyo kutenga taifa hilo la Kiyahudi haswa katika miaka ya 60 na 70 harakati za PLO ziliposhika kasi.
Ziara hii inatarajiwa kupunguza tofauti hizo na kuwapa chambo mataifa ya Afrika iliwalegeze misimamo mikali dhidi ya Israeli.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257