Habari mpya

Waandamanaji wakabiliana na polisi Marekani


Image copyrightGETTY
Image captionWaandamana kupinga mauaji ya weusi Marekani

Polisi katika jimbo la Louisiana Marekani wamemkamata mwanaharakati wa kupigania haki za weusi katika makabiliano na waandamanaji katika mji wa Baton Rouge.

Image copyrightAP
Image captionDeRay McKesson alikuwa mmoja wa waandamanaji waliokamatwa

DeRay McKesson alikuwa mmoja wa waandamanaji waliokamatwa na polisi wakipinga mauaji ya weusi wawili mikononi mwa polisi.

Image copyrightAP
Image captionMapema rais Obama alikana kuwa Marekani imetumbukia katika ubaguzi wa rangi wa miaka 60.

Kamata hiyo ya polisi ilitokea huku maandamano ya kupinga mauaji yanayofanywa na polisi dhidi ya watu weusi yakiendelea katika miji kote nchini Marekani licha ya wito kutoka kwa rais Barack Obama kulitaka taifa kuungana baada ya kuuawa kwa polisi 5 katika mji wa Dallas.

Image copyrightEPA
Image captionMaandamano mengi yalikuwa ya amani.

Maandamano mengi yalikuwa ya amani.
Lakini katika maeneo ya Baton Rouge huko Louisiana na St Paul katika jimbo la Minnesota, maeneo ambapo wanaume wawili weusi waliuawa juma lililopita, kulishuhudiwa makabiliano kati ya polisi na waandamaji.
Mapema rais Obama alikana kuwa Marekani imetumbukia katika ubaguzi wa rangi wa miaka 60.

Image copyrightAP
Image captionPolisi katika jimbo la Louisiana Marekani wamemkamata mwanaharakati wa kupigania haki za weusi

Huko Baton Rouge waandamanaji walikuwa na kibwagizo cha 'no justice, no peace', yaani ''bila ya haki kutendeka hakutakuwa na amani''

Image copyrightAP
Image caption"black lives matter" na "hands up, don't shoot" vilirindima kote

Vibwagizo hivyo pamoja na "black lives matter" na "hands up, don't shoot" vilirindima kote katika maeneo hayo ya hivi punde zaidi kuathirika na mauaji ya weusi.

No comments

+255716829257