Serena ashinda taji la 22 la Grand Slam
Mchezaji wa tenisi nambari moja upande wa wanawake duniani Serena Williams amemshinda mchezaji nambari nne duniani kutoka Ujerumani Angelique Kerber ili kushinda taji la saba la Wimbledon na taji 22 la Grand Slam.
Raia huyo wa Marekani alikabiliana na upepo mkali kushinda seti 7-5 na 6-3 na hivyobasi kusawazisha rekodi iliokuwa ikishikiliwa na Steffi Graf ya kushinda mataji muhimu.
Kerber alimshinda Williams katika mashindano ya Australia Open mnamo mwezi Januari,lakini hakuweza kumshangaza tena katika taji la Grand Slam.
William sasa amemaliza msururu mbaya wa kushindwa katika Grand Slam ulioanza katika taji la Wimbledon mwaka uliopita
No comments
+255716829257