UFARANSA: WATU 80 WAUAWA KATIKA SHAMBULIO..
Zaidi ya watu 80 wameripotiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa.
Lori lililokuwa likienda mwendo kasi lilijiingiza katika mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiangalia maonesho ya fataki kuadhimisha siku ya kitaifa ya Bastille, ambayo huja na shamra shamra kila mwaka.
Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre amesema lori hilo liliendelea kutembea kilo mita mbili kabla ya polisi kumpiga risasi dereva.
Bunduki na makombora yameripotiwa kukutwa ndani ya lori hilo.
Waakazi wa mji huo wa Nice wameshauriwa kutulia majumbani.
Rais Francois Hollande amerudi mjini Paris kwa ajili ya kufanya kikao cha dharura.
Hali ya tahadhari iliyowekwa toka kutokea kwa shambulio lililofanywa na Islamic State mjini Paris, bado iko palepale nchini Ufaransa.
No comments
+255716829257