MISRI: HOSSAM AOKOLEWA NA MWANAE KWENDA JELA..
Mfungaji wa mabao mengi wa mda wote nchini Misri Hossam Hassan ameokoka na kifungo cha jela baada ya mtoto wake wa kike kuandika ujumbe wa kumuombea msamaha katika mtandao wa facebook.
Hassan alitakiwa kufikishwa mahakamani baada ya kumshambulia mpiga picha wa polisi baada ya mchezo kumalizika.
Mpiga picha huyo alisoma ujumbe huo katika mtandao wa facebook na kuondoa kesi hiyo dhidi ya mshambuliaji huyo wa zamani ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Al-Masry.
''Maneno yake yalinifanya nijisikie vibaya sana''Reda Abdelmaged alisema.
Tukio hilo lilitokea baada ya mchezo kati ya Al Masry na Ghazl Al Mahalla uliosha kwa suluhu ya 2-2 ambapo kulikuwa na mchuano kati ya pande hizo mbili.
Licha ya kesi hiyo kuondolewa Hassan ataendelea kubaki kizuizini mpaka muendesha mashitaka afute kesi hiyo.
No comments
+255716829257