Tanzania yapata nafasi ya kuandaa mkutano wa kimataifa wa usalama wa mitandao..
Mkutano wa usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle umefanyika jijini Dar es Salam katika hoteli ya Hyatt ambapo wadau mbalimbali wa masuala ya teknolojia walikutana na kujadili matumizi salama ya mtandao.
Mambo
makuu yaliyojadiliwa katika mkutano huo ambao umefunguliwa na Naibu
Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba, ni
usalama katika matumizi ya mitandao ya teknojia, Usimamizi wa utunzaji
wa data na taarifa za siri na jinsi ya kukabiliana na hasara
zinazotokana na matumizi mabaya ya mtandao yenye kuleta athari kwa
watumiaji.
Imeeleza
katika mkutano huo kuwa kila mwaka mabilioni ya dola hutumiwa na
taasisi mbalimbali kujiweka salama na athari za kimtandao ambapo hata
hivyo imeelezwa kuwa wezi wanaojinufaisha kupitia teknolojia kila
kukicha wanabuni mbinu mpya za kufanya uharifu kupitia katika mitandao
ikiwemo kuiba taarifa za siri kutoka kwenye makampuni na taasisi.
Taarifa
zimebainisha kuwa hivi karibuni wizi wa kimtandao uliosababisha hasara
ya dola za Kimarekani bilioni 300 umefanyika na kiasi cha dola
bilioni100 umefanyika kupitia kadi maalumu za mihamala ya fedha na
malipo, bara la Afrika likiwa moja ya wahanga wa wezi huu wa kimataifa.
Ripoti
ya mwaka huu kutoka taasisi za Verizon kuhusiana na wizi wa kimtandao
imebainisha kuwa kuwa wizi wa siri za makampuni ni wa pili kufanyika
baada ya wizi wa fedha japo makampuni mengi hayajawa na mwamko wa
kuwekeza katika kupambana na tatizo hili kubwa ambalo hivi sasa ni janga
la kimataifa.
Makamu
Rais wa taasisi ya Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na
mapambano dhidi ya wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklicki amesema
kuwa mikakati ya kuzuia wizi huu kuliko athari zinazojitokeza baada ya
kuingiliwa katika mtandao na kuibiwa taarifa za siri za kampuni.
Alisema
wizi huu wa kimtandao ni moja ya changamoto inayozikabili taasisi
mbalimbali na makampuni ya biashara na ndio mwanzo wa kutengenezwa
bidhaa bandia kwenye masoko na alisisitiza kuwa utunzaji wa taarifa za
siri ni jambo la kwanza la msingi kwa kampuni
Mkutano
huo ambao umedhaminiwa za taasisi za Oracle na CIO Afrika na
kuhudhuriwa na watendaji kutoka serikali na taasisi mbalimbali umetoka
na maazimio ya kuhakikisha uwekezaji wa kiteknolojia unafanyika katika
kuhakikisha wizi huu wa kimtandao unadhibitiwa na makampuni kuwa makini
kuhakikisha yanalinda taarifa zake za siri.
Makamu Rais wa taasisi ya
Oracle kanda ya Afrika ambayo inajishughulisha na mapambano dhidi ya
wizi wa kimtandao duniani, Janusz Nacklick (aliyeshika kipaza sauti)
akijibu maswali mbele ya waandishi wa habari wakati wa mkutano wa
usalama wa katika matumizi ya TEKNOHAMA wa Oracle uliofanyika jijini Dar
es Salam katika hoteli
ya Hyatt. Pembeni yake kushoto ni mgeni rasmi aliyefungua mkutano huo
Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Tahaya Simba
pamoja na viongozi wengine. (Picha na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog)
No comments
+255716829257