Habari mpya

OBAMA AWASIHI WAMAREKANI DHIDI YA MASHUMBULIZI YAKIBAGUZI..


Rais Barrack Obama wa Marekani amewasihi wamerakani wajizue dhidi ya hisia kali baada ya Mmarekani Mweusi kuwapiga risasi na kuwaua maafisa watatu wa polisi katika shambulizi la pili la kulipiza kisasi dhidi ya polisi wazungu wanaowaua wamarekani weusi.
Obama ameomba uvumilivu utawale mioyo ya wakaazi wa mji wa Baton Rouge Louisiana nchini Marekani ambao sasa wanahofu ya kuzuka mashambulizi ya kulipiza kisasi.


Image copyrightREUTERS
Image captionGavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliwapiga risasi polisi kulipiza kisasi mauaji ya Alton Sterling

Obama aliyasema hayo katika hotuba ya moja kwa moja kupitia kwa runinga kutoka ikulu ya WhiteHouse muda mchache tu baada ya mtu mmoja mweusi kuua maafisa watatu wa polisi hukohuko Baton Rouge alikouawa mtu mweusi
Alton Sterling pasi na hatia yeyote majuma mawili yaliyopita.


Image copyrightFACEBOOK
Image captionAlton Sterling aliyeuawa na polisi mzungu pasi na kosa lolote

Hasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea kwa muda mrefu ilihali hakuna hatua inayochukuliwa dhidi yao.
Gavin Long ambaye ni mwanajeshi wa zamani alikuwa amerekodi ujumbe katika mji wa Dallas siku chache baada ya polisi watano kuuawa mjini humo katika shambulizi lililotekelezwa kulipiza kisasi cha mauaji ya Sterling.


Image copyrightREUTERS
Image captionHasira imekuwa ikitokota miongoni mwa watu weusi baada ya mtindo wa kuuawa kwa wanaume weusi na polisi wazungu kuendelea kwa muda mrefu

Sasa imebainika kuwa Long alikuwa ameweka video kwenye mtandao akilalamika jinsi polisi wanavyowatendea waamerika weusi ambapo alitoa wito kwa wanaume weusi kujitolea kuokoa jamii yao.
Long mwenye umri wa miaka 29 aliwahi kuhudumu kama mwanajeshi wa Marekani .
Rais Obama ameshauri watu weusi dhidi ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Polisi akisema mauaji ya kulipiza kisasi sio suluhisho la tatizo sugu la ubaguzi wa rangi bali utachochea uhasama zaidi dhidi yao na polisoi wazungu

No comments

+255716829257