SUMAYE AREJESHA FOMU YA UENYEKITI CHADEMA..
Waziri mkuu mstaafu wa serikali ya awamu ya tatu Frederick
Sumaye amerudisha fomu ya kuwania nafasi ya uenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ kanda ya Pwani, Sumaye ana wapinzani
wawili ambao ni John Gugunita na Gango Kidera.
Nafasi
zingine za uongozi ambazo zipo wazi ni makamu mwenyekiti ambapo watu
watatu wamejitokeza kugombea nafasi hiyo akiwemo Saed Kubenea, nafasi ya
mwekahazina wagombea watatu wamejitokeza akiwemo aliyekuwa naibu waziri
wa kazi na ajira wa serikali ya awamu ya nne, Makongoro Mahanga.
No comments
+255716829257