Habari mpya

PERUZI HABARI KUU ZA ULIMWENGU LEO JULY 11, 2016..

Shinzo Abe ashinda uchaguzi Japan

Matokeo ya mwisho katika uchaguzi wa jana nchini Japan yanaonyesha kuwa serikali ya muungano ya waziri mkuu, Shinzo Abe, umeshinda theluthi mbili iliyo muhimu katika bunge kuu.
Inampa bwana Abe nafasi ya kuikarabati katiba inayopinga vita nchini humo.

Mshambuliaji wa Dallas alipanga makubwa



MicahImage copyrightAFP
Image captionMicah Johnson

Mkuu wa polisi katika mji wa Dallas Marekani amesema mshambuliaji aliyewapiga risasi maafisa watano wa polisi na kuwaua, alikuwa anapanga shambulio kubwa zaidi. Amesema wamepata ushahidi kuwa Micah Johnson alifanya majaribio ya kulipuwa vilipuzi.

Waziri wa Misri aitahadharisha Israel



Image copyrightGETTY

Waziri wa mambo ya nje wa Misri , Sameh Shoukry, ameonya kuwa uwezekano wa kupatikana amani na usalama unafifia kwa Israeli ili mradi mzozo na raia wa Palestina unaendelea.
Aliyasema hayo katika ziara iliyo nadra nchini Israeli, inayotokea wakati Israel imeahidi takriban dola milioni 13 kwa ujenzi wa makazi ya walowezi katika ukingo wa magharibi.

Maafisa wa Israel kumchunguza Netanyahu



Image copyrightAP

Wizara ya haki Israeli inasema mkuu wa sheria nchini humo ameagiza uchunguzi dhidi ya inachokitaja kuwa masuala yanaomhusu waziri mkuu Benjamin Netanyahu. Imetoa taarifa kidogo lakini imesisistiza kuwa sio uchunguzi wa kihalifu. Msemaji wa waziri mkuu ameeleza kuwa uchunguzi huo hautobaini chochote.

Korea Kaskazini kujibu hatua ya Marekani



Image copyrightEPA

Jeshi la Korea kaskazini linasema litachukua hatua za nguvu dhidi ya kutumwa kwa mfumo wa hali ya juu kutoka Marekani kuzuia makombora angani Korea Kusini.
Limesema litachukua hatua punde litakapofahamu wakati na sehemu ambapo makombora hayo yatatumwa.
Maafisa Korea Kusini watadhibitisha katika wiki kadhaa sehemu ambapo makombora hayo yatatumwa.

No comments

+255716829257