Habari mpya

JAMBAZI ALIETOROKA MIKONONI MWA POLISI JIJINI MWANZA AZUA HOFU KWA WAKAZI..

Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza wamekumbwa na hofu kuhusu usalama wa maisha yao baada ya mmoja kati ya majambazi aliyehusika na mauaji ya waumini watatu katika msikiti wa Rahman na kufanya uhalifu katika maduka ya M-Pesa, Tigo-Pesa, Airtel Money, Hamis Juma (38) kutoroka chini ya ulinzi wa askari  Polisi.
Tukio hilo ambalo lilitokea Julai 3 mwaka huu, saa 2:00 usiku katika eneo la mlima Kiloreli Nyasaka, Manispaa ya Ilemela, limeibua hofu kwa wakazi wa jiji hilo kutokana na mfululizo wa matukio ya uhalifu wakidai kushangazwa na jambazi huyo kuwatoroka Polisi.
Baadhi ya wananchi, walihoji kuwa askari wa idara ya upelelezi walijiamini vipi kwenda na jambazi huyo mafichoni kwa wenzake bila kuwa na ulinzi wa kutosha kumfunga pingu za miguu, mikono.
Tulitilia mashaka tukio hili kutokana na matukio yanayoendelea kutokea, tumezoea kuona polisi wakiwafunga pingu za mikono au miguu watuhumiwa mbalimbali wanaokamata hata kama hana madhara, iweje jambazi asifungwe pingu
”Jambazi aliyetoroka ameshiriki tukio kubwa la kuuawa watu wasio na hatia, watuhumiwa wa matukio ya kigaidi hupelekwa na mahakamani chini ya ulinzi mkali wa polisi wenye silaha nzito’
Akijibu tuhuma hizo, kamanda wa Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi alisema tukio hilo lilikua la ghafla, polisi ni binadamu, wakiwa njiani kwenda mafichoni ghafla majambazi walianza kuwashambulia ikabidi wachukue tahadhari ili kujihami na mashambulizi kwa kujibizana nao risasi ndipo jambazi huyo akatoroka.

No comments

+255716829257