Habari mpya

Murray amchapa Lu michuano ya Wimbledon

 
Mchezaji namba moja wa Tennis nchini England Andy Murray amemshinda Yen-Hsun Lu katika ushindi wa moja kwa moja na kufanikiwa kutinga mzunguko wa tatu katika michuano ya Wimbledon.
Murray ameshinda kwa seti 6-3 6-2 6-1 hivyo atakutana na John Millman kutoka Australia ambaye amemshinda Benoit Paire wa Ufaransa.
Lu kutoka Taiwan anayeshikilia nafasi ya 76 duniani, ameshinda michezo 11 katika michuano mbalimbali kabla ya kufungwa na Murray.
''Mchezo ulikuwa mgumu hususani kwenye seti ya kwanza,''alisema Murray mwenye miaka 29.
Wakati huohuo Garbine Muguruza kutoka Venezuela ameondolewa katika michuano hiyo baada ya kukubali kipigo cha seti 6-3 6-2 kutoka kwa Jana Cepelova wa Slovakia.
Cepelova atakutana na Lucie Safarova katika mzunguko wa tatu.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257