ITAKUWA NDOTO KWA MASHABIKI KUINGIA BURE TENA UWANJA WA TAIFA BAADA YA YANGA VS TP MAZEMBE..
Baada ya mechi kati ya Young Africans na TP Mazembe iliyochezwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kupoteza kwa goli 1-0 imeibua mapya, kutokana na kitendo cha Yanga kuamua mechi hiyo mashabiki waingie bure uwanjani.
Kitendo hicho cha Yanga ambacho kinatajwa kuhatarisha maisha ya mashabiki waliojitokeza na miundombinu ya uwanja, shirikisho la soka Tanzania TFF limetangaza kupitia Rais wake Jamal Malinzi kuwa,
kuanzia sasa mechi zote za kimataifa hazitoratibiwa tena na vilabu,
kitendo ambacho kinatafsiriwa kama hakutatokea tena mashabiki kuruhusiwa
kuingia bure uwanjani.
“Nimewaita
kutokana na hali isio ya kawaida iliyojitokeza katika mchezo kati ya
Yanga na TP Mazembe, TFF ndio chombo chenye mamlaka ya kuratibu michuano
ya ndani na kimataifa yanayohusisha timu za Tanzania, kutokana na
kitendo walichofanya Yanga, TFF imeamua kuwa itakuwa inaratibu mechi
zote na sio tena vilabu” Alisema Malinzi.
No comments
+255716829257