DIEGO COSTA KUSALIA CHELSEA..
Meneja mpya wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amesema mshambuliaji Diego Costa atasalia katika klabu hiyo msimu ujao.Amesema amemjumuisha kwenye mipango yake.
Costa amehusishwa na kuhamia klabu yake ya zamani Atletico Madrid baada ya kutofana sana msimu uliopita.
Mchezaji huyo wa umri wa maka 27 amefungia Chelsea mabao 36 katika mechi 77 tangu ajiunge nao 2014.
"Diego anasalia nasi. Anatia bidii sana. Ana furaha kufanya kazi na wachezaji wenzake na mimi pia,” amesema Conte.
"Yeye ni mchezaji mzuri sana, mchezaji muhimu, na kwa hivyo hakuna tatizo.
"Yeye ni mchezaji mzuri, mmoja wa wale bora duniani, na nina uhakika kwamba yumo kwenye mipango yetu na atatufungia mabao mengi.”
No comments
+255716829257