JIJI LA RIO DE JANEIRO LAFULIA KABLA YAKUANZA KWA OLIMPIKI..
Gavana wa Jiji la Rio de Janeiro
amesema kuwa jimbo lake limeishiwa na fedha za kutoa huduma za umma -
siku hamsini tu kabla ya kuanza michezo ya Olimpiki.
Francisco
Doernelles amesema kwamba amelazimika kutangaza hali ya hatari ya
kifedha ili kuomba Serikali Kuu ya Brazil kusaidia katika juhudi za
kuandaa michezo hiyo.Alisema hali ya kifedha ya sasa inaweza kuzuia Rio kutekeleza majukumu yake katika michezo ya Olimpiki ya walemavu.
Hatua madhubuti zinatekelezwa katika utoaji huduma wa usalama, uchukuzi na huduma zingine za umma.
Alisema bila msaada wa aina hiyo shughuli zote za uandaaji wa michezo hiyo zitaporomoka.
Rais Michel Temer, aliyetembelea Rio juma hili alisema kuwa atahakikisha kuwa huduma zote zinazohitajika zinatekelezwa.
chanzo: BBC
No comments
+255716829257