Habari mpya

HUSSEIN MACHOZI ANATARAJIA KUJIUNGA NA LEBO YA MAN WALTER..

 Image result for hussein machozi
Hussein Machozi amefafanua taarifa za kufanya kazi na mtayarishaji wa muziki, Man Walter ili aweze kurudi kwenye ubora wake kama ilivyokuwa zamani.
Ni kipindi kirefu Machozi amekuwa kimya japo ameweza kuachia nyimbo kadhaa lakini bado hazikuweza kufanya vizuri.
Akiongea na Bongo5, Hussein Machozi amesema kuwa mikakati ikikaa sawa atahamia kufanya kazi na Man Walter kama lebo.
“Mikakati kiukweli tuliipanga lakini mpaka sasa hivi hatujapanga lolote, sidhani kama itaweza kukamilika. Kuna makubaliano mazuri tuliaza kuyafanya. Lakini kama ikikaa sawa mimi na Walter tutafanya kazi zote na mipango yangu yote itahamia kwake, nitakuwa kama lebo pale,” alisema Machozi.
CHANZO: Bongo5

No comments

+255716829257