Habari mpya

DOGO MFAUME NAYE AKIRI KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA..

 
Mahindi wa KTMA mwaka 2010 kupitia kipengele cha wimbo bora wenye vionjo vya asili na hit maker wa "KAZI YA DUKA" Dogo Mfaume amekiri kuwa alikuwa anatumia dawa za kulevya kwa kipindi cha miaka miwili sasa.
Akifanya mahojiano na Perfecto Tv, Dogo Mfaume amsema kuwa vijana wengi hujikuta wakiingia katika dimbwi la matumizi hatari ya dawa za kulevya kutokana na vishawishi vya marafiki na pamoja na fikra potofu hasa za kuamini kuwa madawa hayo huongeza hamasa ya mapenzi.
Hata hivyo Dogo Mfaume amesema kuwa ameamua kuacha rasmi matumizi ya dwa hizo pamoja na kutoa rai kwa vijana wenzake na watu wote wanaotumia dawa hizo hatari kwa afya zao kuwa na moyo kama wake wakuamua kuacha.

No comments

+255716829257