Waandishi wawekwa korokoroni Misri
Mamlaka nchini Misri imeamuru kuwekwa kizuizini kwa waandishi wawili wa habari kwa wiki mbili, kwa shutuma za kuchochea maandamano.
Wakosoaji wawili wa serikali Amr Badr na Mahmud el-Sakka walizuiliwa kuingia makao makuu ya waandishi wa habari nchini Misri na polisi waliokuwa wamevalia nguo za kiraia.
Taarifa kutoka kwa mwendesha mashitaka wa umma inasema waandishi hao wawili wanashutumiwa kusambaza taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii wakishawishi mashambulizi dhidi ya polisi na wafanyakazi wa jeshi kwamba wanamiliki silaha za moto.
Muungano wa waandishi wa habari nchini Misri umetoa wito kwa kufukuzwa waziri wa mambo ya ndani.
CHANZO: BBC
No comments
+255716829257