Habari mpya

Trump asema Uchina “inaibaka” Marekani

TrumpImage copyright
Image captionTrump amekuwa akisema sera za Uchina zinaiumiza Marekani
Mgombea mkuu wa chama cha Republican Donald Trump ameshutumu Uchina na kusema imekuwa “ikiibaka” Marekani kupitia sera zake za kibiashara.
Ameambia watu waliohudhuria mkutano wa kisiasa Indiana kwamba Uchina imekuwa ikitekeleza “wizi mkubwa zaidi kuwani kutekelezwa katika historia ya dunia.”
Bw Trump, mfanyabiashara tajiri kutoka New York, amekuwa akiituhumu Uchina kwa kuchezea sarafu yake ili kuwa na ushindani wa kibiashara duniani inapouza bidhaa nje ya nchi.
Hilo, amesema, limeathiri sana wafanyabiashara na wafanyakazi wa Marekani.
“Hatuwezi kuruhusu Uchina iendelee kuibaka nchi yetu, na hilo ndilo tunafanya (kwa wakati huu),” alisema mkutanoni Jumapili.
"Tutabadilisha mambo, na tuna uwezo, msisahau. Tuna nguvu sana dhidi ya Uchina.”
Katika manifesto yake ya kampeni, Bw Trump ameahidi kufanikisha mkataba bora wa kibiashara baina ya Uchina na Marekani ambao utawezesha “wafanyabiashara na wafanyakazi kutoka Marekani kuweza kushindana”.
Ametaja malengo manne ambayo yanahusisha kutangaza Uchina kuwa taifa linalochezea sarafu yake na kusitisha utoaji wa nafuu za wafanyabiashara wanaouza bidhaa nje ya nchi ambazo anasema ni haramu.
Aidha, anaitaka Uchina kufikisha kikomo mfumo duni wa masharti ya leba na uhifadhi wa mazingira.
TrumpImage copyrightAFP
Image captionMamia ya watu waliandamana kumpinga Trump California Ijumaa
Takwimu za karibuni zaidi kutoka kwa serikali ya Marekani zinaonesha pengo la kibiashara baina ya Uchina na Marekani lilipanda na kufikia $365.7bn (£250.1bn) mwaka jana. Kufikia Februari mwaka huu, pengo hilo lilikuwa limefika $57bn tayari.
Hii ni mara ya kwanza kwa Trump kutumia neno “ubakaji” akizungumzia biashara na Uchina, lakini amejulikana kwa kutumia maneno makali kwenye kampeni yake.
Alikabiliwa na mamia ya waandamanaji jimbo la California Ijumaa kabla yake kutoa hotuba katika mkutano wa chama cha Republican Ijumaa.
Alilazimika kutumia mlango wa nyuma kuingia.
Waziri mkuu wa Uchina Li Keqiang amesema Wachina wanafuatilia kwa karibu uchaguzi nchini Marekani.
Hata hivyo anasema wengi wanamtazama Bw Trump kama mtu wa kuenziwa badala ya adui.
chanzo: BBC

No comments

+255716829257