Habari mpya

Mirror kuachia kolabo yake na Ommy Dimpoz

Msanii wa muziki kutoka label ya Wema SepetuEndless Film, Mirror anajipanga kuachia kolabo yake na Ommy Dimpoz.

 Meneja wa msanii huyo kutoka Endless FilmPetitman Wakuache, amesema Mirror ni msanii ambaye style yake ya uimbaji haiwezi kufananisha na wasanii mwingine.
Mirror ni msanii mzuri sana na muziki wake hauwezi kuufananisha na wa wasanii wengine, kwa hiyo watu msione kimya, kuna kolabo mpya Ommy Dimpoz itatoka, pia kuna video mpya ambayo tumeshoot Afrika Kusini. Kwa hiyo mashabiki wasione watu hawafanyi kazi, wakati kazi wanaziona, wao wanatakiwa wasupport kazi zilizopo kwanza,” alisema Petit.
Pia Petit alisema Mirror ni msanii ambaye hauwezi kumfananisha na wasanii mwingine, kwani muziki wake unaishi muda mrefu.

chanzo: Djmwanga

No comments

+255716829257