MANCHESTER UNITED WASHINDA KOMBE LA FA..
Manchester United wameshinda Kombe la FA baada ya kuwalaza Crystal Palace 2-1 katika fainali iliyochezewa uwanja wa Wembley.
Ni mara yao ya kwanza kushinda kikombe hicho tangu 2004.
Mabao ya Manchester United yalifungwa na Juan Mata na Jesse Lingard.
Bao la kufutia machozi la Crystal Palace limefungwa na Jason Puncheon.
Ushindi huo ni nafuu sana kwa meneja wa Manchester United Louis van Gaal ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutokana na kutofana kwa klabu hiyo.
Kwa ushindi huo, Manchester United wamefikia rekodi ya Arsenal kwa kushinda kombe hilo mara 12.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, Van Gaal alisema amefurahia sana kushinda kikombe hicho.
"Ni muhimu sana kushindia klabu kikombe hiki, kwaa mashabiki, na mimi pia kwa sababu sasa nimeshinda katika mataifa manne, na si mameneja wengi wamefanikiwa kufanya hivyo," amesema.
"Tukiwa na wachezaji 10, na tulikuwa tumecheza Jumanne jioni pia, lakini tulistahiki. Lilikuwa bao zuri sana, sio?"
22:08 Mechi inamalizika.
22:08Jesse Lingard anaupata mpira.
22:05 Zaha anajaribu bahati tena, lakini hafanikiwi.
22:00 Zaha anashambulia lango ya United. Anagongana na kipa De Gea ambaye anaudaka mpira. De Gea anaonekana kuumia.
21: 57 Mile Jedinak anatoa kombora hatua 20 kutoka kwa goli, anakaribia kufunga lakini hafanikiwi.
21:56 BAOOOOO! Manchester United wanafunga. Man Utd 2-1 Palace
Bao limefungwa na Jesse Lingard.
21:55 Michael Carrick anapata nafasi nzuri. Lakini mpira wake unatoka nje.
21:54 Lingard anajaribu kuanzisha shambulio upande wa United, anaangushwa na McArthur ambaye anaoneshwa kadi ya njano.
21:52 Palace wanashambulia, Gayle anatoa kombora lakini De Gea anaokoa, Bolasie anajaribu tena. Mwishowe mpira unatoka nje na inakuwa kona. Haizai matunda.
21:52 Kipindi cha pili muda ziada chaanza.
21:49 Ni wakati wa mapumziko muda wa ziada.
21:47 Kadi Nyekundu
Smalling anaoneshwa kadi ya pili ya njano.
21:44 Yannick Bolasie anatoa mpira safi, De Gea anaugusa kidogo na kuutema nje. Inakuwa kona, lakini haizai matunda.
21:41 Fellaini anashambulia, mpira unazuiwa lakini Lingard anajaribu tena. Inakuwa kona.
21:35 Wilfried Zaha anashambulia lakini anaangushwa na Daley Blind. Palace, wanataka penalti lakini hawapati.
21:35 Kipindi cha kwanza muda wa ziada.
21:27 Muda wa kawaida unamalizika. Ni mapumziko kabla ya muda wa ziada kuanza.
21:26 Zaha anapata nafasi nzuri. Lakini mpira wake unapita nje ya lango.
21:25 Scott Dann anatolewa uwanjani na nafasi yake anaingia Adrian Mariappa.
21:22 Juan Mata anatolewa uwanjani. Nafasi yake anaingia Jesse Lingard.
21:21 Palace wanapata kona mbili, lakini hawafanikiwi kufunga.
21:19 Wayne Rooney anafanya madhambi na kuonyeshwa kadi ya njano.
21:18 Mshambuliaji wa Palace Wickham anatolewa uwanjani. Nafasi yake anaingia Dwight Gayle.
21:12 BAOOOOO! Mata anasawazishia Manchester.
21:09 BAOOOOO! Puncheon anafunga.
21:07 Palace wanashambulia. Lakini Wickham anaangushwa na Valencia. Palace wanapewa mpira wa adhabu.
21:04 Jason Puncheon anaingia nafasi ya Yohan Cabaye upande wa Palace.
21:04 Ashley Young anaingia nafasi ya Rashford.
21:03 Cabaye anashambulia, lakini mwamuzi anasema ameotea.
21:02 Marcus Rashford anakabiliwa na Mfaransa Yohan Cabaye na kuumia. Baada ya muda anaondoka uwanjani.
22:58 Rojo anatolewa uwanjani na nafasi yake anaingia Matteo Darmian.
20:54 Marcus Rojo anaumia. Anatolewa nje lakini baada ya muda kidogo anarejea uwanjani na kuendelea kucheza.
20:50 Anthony Martial anatoa mpira safi wa kichwa. Lakini Palace kwa mara ya pili wanaokolewa na mlingoti wa goli.
20:45 Bolasie naye anashambulia upande ule mwingine. Lakini hafanikiwi.
20:44 Fellaini anapata mpira mzuri eneo la hatari kutoka kwa Rashford, lakini linazuiwa na mlingoti wa goli.
20:40 Scott Dann ndiye mchezaji wa kwanza wa Palace kuadhibiwa. Anapewa kadi ya njano kwa kumwangusha Marcus Rashford.
20:37 Kipindi cha pili kinaanza.
- Manchester United 0-0 Crystal Palace
20:21 Ni wakati wa mapumziko.
20:19 Juan Mata wa United anaoneshwa kadi ya njano kwa kumchezea visivyo Pape Souare.
20:15 Crystal Palace wanashambulia tena lakini refa Mark Clattenburg anarejesha mchezo nyuma. Joel Ward alifanyiwa madhambi na Marcos Rojo analishwa kadi ya njano.
20:10 Wilfried Zaha anapata mpira na kukimbia nao lakini anakabiliwa na Wayne Rooney, anaanguka.
20:08 Anthony Martial anapata krosi safi kutoka kwa Marcus Rashford eneo la hatari, lakini kombora lake linazimwa na Joel Ward .
20:02 Yannick Bolasie anapata fursa na kutoa kombora kali. De Gea anaokoa.
19:59 United wanapata kona. Fellaini anakaribia kufunga kwa kichwa, lakini mpiga unatolewa nje. Inakuwa kona nyingine lakini haizai matunda.
19:57 Mata anatoa kombora kali. Linatulizwa kidogo na kipa Hennessey lakini mpira bado unasonga. Mchezaji wa Palace anaufagia na kuuondoa hatarini.
19:53 Mpira wa adhabu unapigwa na Yohan Cabaye na Yannick Bolasie anaugusa kwa kichwa na karibu utue wavuni lakini De Gea anautupa juu ya wavu.
19:52 Mchezaji wa Palace Wickham anakabiliwa na Smalling, anaangushwa lakini anajinyanyua na kufunga. Lakini bao linakataliwa. Mwamuzi anarejesha mpira nyuma na unakuwa mpira wa adhabu. Smalling anapewa kadi ya njano.
19:51 Rooney kutoka nje ya eneo la hatari anatoa krosi safi kwa Marcus Rojo ambaye anatoa kombora. Lakini kipa wa Palace Hennessey anaudaka.
19:49 Rooney anatoa kombora ambalo kidogo linamzidi kipa wa Palace anayeutema lakini baadaye anafanikiwa kuufikia.
19:48 David de Gea analazimika kutumia ujanja kuzuia mpira kutoka nje.
19:45 Rashford anapata mpira eneo la hatari, anatoa kombora lakini linazuiwa na inakuwa kona. Fellaini anajaribu kuufikia mpira kwa kichwa bila mafanikio.
19:43 United wanapata kona nyingine, hii inapigwa juu lakini haizai goli.
19:41 Rashford anajikakamua kupitia winga na kujaribu kuelekea kwenye lango la Palace. Anakabiliwa Damien Delaney na kutoa mpira nje. Lakini Palace wanazawadiwa kona ambayo inapigwa fupi.
19:40 United wanapata kona. Inapigwa kona fupi. Lakini haizai matunda.
19:39 Palace wanapata kona. Lakini mpira unatua mikononi mwa De Gea.
19:38 Klabu zote mbili zinashambulia.
19:35 Mechi inaanza.
19:30 Mwanamfalme William anawasalimia wachezaji wote 22.
19:29 Wachezaji wanaingia uwanjani.
18:59 Wachezaji kwa sasa wanapasha misuli moto. Mechi itaanza saa moja unusu. Kuna dakika 30 hivi kabla ya kipenga cha kwanza kupulizwa.
18:33 Wachezaji watakaoanza mechi leo wametangazwa.
Manchester United wamefanya mabadiliko mawili, Marouane Fellaini amerejea kikosini.
Kikosi cha Man Utd: De Gea, Valencia, Smalling, Blind, Rojo, Carrick, Fellaini, Mata, Rooney, Martial, Rashford
Crystal Palace: Wilfried Zaha anaanza mechi hii ya Wembley.
Kikosi cha Palace: Hennessey; Ward, Dann, Delaney, Souare; Zaha, Cabaye, McArthur, Jedinak, Bolasie; Wickham.
18:31 Mechi ya leo ni kama marudio ya fainali ya 1990. Mechi ya kwanza timu hizo zlitoka sare 3-3 lakini mechi ya marudiano, Manchester United wataondoka na kikombe baada ya kushinda 1-0.
18:30 (Saa za Afrika Mashariki): Hujambo na karibu kwa matangazo ya moja kwa moja ya Fainali ya Kombe la FA.
Manchester United wanashuka dimbani dhidi ya Crystal Palace uwanjani Wembley.
No comments
+255716829257