Habari mpya

KIWANDA CHA MBOLEA KUJENGWA MKOANI LINDI..

TanzaniaImage copyrightSTATEHOUSE TANZANIA
Image captionKiwanda hicho kitagharimu dola bilioni 3 za Kimarekani
 Serikali imetangaza kwamba inatarajia kuanza ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha mbolea mwaka huu.
Kiwanda hicho kitajengwa katika wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi na kitatumia rasilimali ya gesi asili na miamba ya matumbawe (coral reefs) iliyopo wilayani Kilwa.
Kitajengwa kwa ubia kati ya Tanzania na nchi za Denmark, Ujerumani na Pakistani na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 3,800 za mbolea kwa siku.
Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania Egon Kochanke na balozi wa Denmark Eina Hebogrd waliokutana na Rais John Magufuli Alhamisi na kujadili ujenzi wa kiwanda hicho.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu, kiwanda hicho kitatosheleza mahitaji ya wakulima nchini na nyingine kuuzwa nje ya nchi.
Aidha, kinatarajiwa kuzalisha ajira zaidi ya 5,000 na uwekezaji wake utagharimu dola za Kimarekani bilioni 3.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257