Habari mpya

MABASI YA MWENDO KASI YAMEANZA KUTOA HUDUMA RASMI JIJINI DAR..

Image captionMabasi ya mwendo wa kasi Dar es salaam..
Huduma ya mabasi ya uchukuzi yanayoenda kwa kasi BRT imeanza rasmi siku ya jumanne katika jiji la Dar es Salaam.
Abiria watalipa shilingi 400 na 800 huku wanafunzi wakilipa 200 kulingana na mamlaka ya uchukuzi wa barabarani na majini SUMATRA.
Image captionKituo cha mabasi ya mwendo wa kasi 
Mkurugenzi mkuu anayesimamia mamlaka hiyo bw Giliard Ngewe amewaambia maripota kwamba nauli zitakuwa shilingi 400 kwa uchukuzi wa barabara ndogo,650 kwa barabara kuu na shilingi 800 kwa uchukuzi wa barabara kuu na ndogo huku wanafunzi wakilipa shilingi 200 kwa kila safari.
Image captionAbiria wakiwa wamepanda basi la BRT
Siku ya Jummanne na Jumatano mabasi hayo yatahudumu kati ya saa kumi na moja alfajiri na saa sita mchana.
Image captionKituo cha mabasi ya BRT 
"Tunawaonya wanaoendesha pikipiki na madereva wa magari mengine kutotumia barabara za mradi wa BRT",alisema akiongezea kwamba bado wanazungumza na washikadau kutafuta njia nzuri ya kupanga barabara zitakazotumiwa na BRT na mabasi mengine ya abiria.
Kulingana na yeye,mfumo huo wa BRT hauyaruhusu mabasi mengine kutoa huduma pamoja na mabasi ya BRT kwa hivyo abiria walioko katika barabara za BRT hawataruhusiwa kutumia mabasi mengine.

No comments

+255716829257