Habari mpya

MABAKI YA NDEGE NA VIUNGO VYA BINADAMU VYAPATIKANA BAHARI YA MEDITERRANEAN..

Image copyrightGETTY
Mabaki ya ndege na vipande vya wanadamu vimepatikana vikielea kwenye Bahari ya Mediterranean na makundi yanayotafuta ndege ya kampuni ya EgyptAir iliyotoweka Alhamisi.
Waligundua pia viti na mizigo ya abiria.
Katika muda wa maaa machache yaliyoipita takwimu zinaonyesha kuwa vingora vya kuashiria kwamba moshi upo, vilianza kulia kabla ya ndege hiyo kutoweka ikiwa na abiria 66.
Image copyrightAFP
Image captionFamilia za waathiriwa wa ajali ya ndege
Mwandishi wa BBC wa maswala ya Usalama anasema kuwa ajali hiyo huenda ikawa ni ya kawaida au ilisababishwa ns mlipuko . Hata hivyo alisema uhakiki hauwezi kujulikana kwa sasa hadi chombo maalumu cha kunasa mawasiliano kwenye ndege kitakapopatikana na kuchunguzwa.
Mjini Cairo ambapo ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Paris, Ufaransa ilikuwa ikitarajiwa, jamaa na marafiki ya abiria wamefanya ibada maalum katika misikiti.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257