Habari mpya

Lewis Hamilton apoteza ushindi

Image copyrightPA
Image captionLewis Hamilton,wa mbio za Langa langa
Dereva Lewis Hamilton anahofia matatizo ya kutokuaminika kwa injini ya ya gari analolitumia kuwa inaweza kuwa sababu ya kutomfikia hasimu wake anayetumia gari la Mercedes Nico Rosberg.
Hamilton yupo alama 43 nyuma ya Rosberg baada ya kumaliza wa pili katika michuano ya jana jumapili ya Russian Grand Prix. Muingereza huyo alisema'' wasiwasi wangu sio kumshinda Nico.Wasiwasi wangu ni iwapo nitaweza patiwa gari litakalonifanya nishindane sawasawa.''
"Je, haitaweza kutokea tena? Hapana kutakuwa na matatizo mbeleni." Sikia: 'Hali ya kukata tamaa inaanza kumkumba Hamilton'Maneno ya Hamilton yanaashiria mlolongo wa matatizo ambayo yamekuwa yakimkumba katika michuano miwili iliyopita.
Nchini Urusi,kufeli kwa injini kulimfanya akamaliza akiwa nambari kumi.Baadaye alijaribu tena kupambana zaidi na kushika nafasi ya pili baada wataalamu wa gari lake walilifanyia marekebisho usiku kucha.
Image copyrightGetty
Wiki mbili zilizopita nchini China pia alikumbwa na tatizo la injini na kumfanya ashindwe kushiriki vizuri,akimaliza nafasi ya saba huku gari lake likiishia kuharibika.
Alianza pia vibaya katika mashindano mawili tofauti nchini Australia na Bahrain yaliyomfanya kuishia nambari mbili na tatu.Rosberg ameshinda katika mbio zote nne alizoshiriki msimu huu.
CHANZO: BBC

No comments

+255716829257