JE DANIEL CRAIG ATAIGIZA KWENYE FILAMU YA JAMES BOND.."007"..?
Mwigizaji mashuhuri Daniel Craig bado hajaamua iwapo ataendelea kuigiza kwenye filamu nyingine ya James Bond, ajulikanaye kama 007.
Kumekuwa na taarifa zilizodokeza kwamba mwigizaji huyo, aliyeigiza kama James Bond katika filamu nne, amekataa nafasi ya kuigiza katika filamu nyingine.
Lakini duru za kuaminika zimeambia BBC kwamba Craig bado hajafanya uamuzi kuhusu 007.
Aidha, huenda asifanye uamuzi huo “hivi karibuni”.
Mapema mwaka huu, MGM, wanaomiliki haki za kibiashara za 007, waliambia wawekezaji kwamba filamu za James Bond zitakuwa zikitolewa kwa mzunguko wa miaka mitatu au minne.
Filamu ya majuzi zaidi, Spectre, ilizinduliwa mwaka 205.
Hii ina maana kwamba filamu ijayo inatarajiwa 2018 au baadaye
CHANZO: BBC
No comments
+255716829257