Habari mpya

IBRA DA HUSTLER AELEZEA MADAWA YA KULEVYA YALIVYOMUATHIRI..

Rapper wa kundi la Nako 2 Nako, Ibra Da Hustler, amewataka wasanii wenzake kukaa mbali na matumizi ya Madawa ya kulevya.
Ibra Da Hustler
Rappa huyo ambaye alikaa rehab kwa muda mrefu ili kusaidiwa kuacha matumizi ya Madawa ya kulevya, amesema kuwa matumizi ya Madawa ya kulevya yamesabisha apoteze dira ya maisha yake.
“Kusema kweli Madawa ya kulevya yamenirudisha nyuma sana, sitaki kuzungumza mengi nadhani hilo liko wazi,” alisema Ibra.
“Mimi sikuwa hivi, niweyumba sana, ndio maana napenda kusema kila kitu kwenye maisha kinatokea kwa sababu, na wenzangu wajifunze kupitia mimi, na kwa wale wenzangu ambao walikubwa na matatizo kama yangu,” aliongeza.
Ibra amesema kwa sasa ameacha kabisa matumizi ya Madawa ya kulevya huku akidai sasa hivi anatumia pombe na sigara tu.
chanzo: Bongo5

No comments

+255716829257