GADNER APINGA KUMDHALILISHA JAYDEE..
Gardner G Habash hawezi kumuomba radhi Lady Jaydee kama ambavyo mwanasheria wa muimbaji huyo alimtaka afanye hivyo ndani ya siku saba kwa madai ya kufanyiwa udhalilishaji.
Mtangazaji huyo wa Clouds FM anawakilishwa na kampuni ya mawakili ya Brevis Attorneys ambao kupitia barua yao kwa kampuni inayomwakilisha Jaydee kwenye madai yake ya kudhalilishwa, Law Associates amedai hakuongea lolote la kumchafua mke wake huyo wa zamani.
“Madai yenu yanapingwa vikali. Mteja wetu hakusema neno, maneno, kauli, sentensi na wala hakuongea kitu cha kuchafua chenye lengo la kuchafua jina na hisia za mteja wako,” wameandika Brevis Attorneys kwenye maelezo yao kwenda kwa mwanasheria wa Jide, Amani Tenga.
“Kwamba tofauti na madai ya mteja weko, katika muda wote wakati wa huduma yake kama MC, mteja wetu hakutaja jina la mteja wako na hivyo madai yako kuwa amemchafua mteja wako hayana msingi wowote,” wameongeza.
Kwenye barua hiyo iliyotolewa Alhamis hii, kampuni hiyo imeishauri Law Associates kusoma upya sheria zinazohusiana na kauli kuhusu ndoa zilizovunjika ‘kuepuka kumpotosha mteja wako.’
“Tafadhali zingata kuwa mteja wetu anayakanusha madai yote ya mteja wako. Iwapo mteja wako ataamua kuendelea na madai au uamuzi katika jambo linalotishiwa, tuna maelekezo thabiti kupinga madai yoyote kwa hasara ya mteja wako mwenyewe yaani gharama na mengineyo.”
Lady Jaydee alimtaka Captain amuombe radhi baada ya kuvuja kwa video inayomuonesha ex wake huyo akiwa MC kwenye shindano la Miss TIA akitamka maneno: “My name is Captain Gardiner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.”
Video hiyo ilisababisha hisia tofauti kwakuwa wengi waliamiani Gardner alimlenga Jaydee.
chanzo: Bongo5
No comments
+255716829257