Habari mpya

Tetemeko la pili la ardhi yatikisa Ecuador

TetemekoImage copyrightPaul Mena Erazo
Image captionTetemeko la kwanza Jumamosi lilisababisha uharibifu mkubwa
Tetemeko jingine la ardhi limetokea katika pwani ya Ecuador, chini ya wiki moja baada ya tetemeko jingine kuua karibu watu 600.
Hakujaripotiwa taarifa zozote kuhusu uharibifu baada ya kutokea kwa tetemeko hilo la nguvu ya alama 6 katika vipimo vya Richter.
Hata hivyo watu wamelazimika kutoka kwenye nyumba zao kama tahadhari.
Tetemeko hilo limetokea baharini kutoka pwani ya eneo la katikati mwa Ecuador lakini hakujatolewa tahadhari yoyote ya kutokea kwa kimbunga.
Serikali ya Ecuador ilisema Jumatano kwamba inapata kutafuta dola bilioni moja za Kimarekani kufadhili juhudi za ukarabati kufuatia uharibifu uliotokana na tetemeko la kwanza lililotokea Jumamosi.
TetemekoImage copyrightPaul Mena Erazo
Image captionWatu wengi wameachwa bila makao
Moja ya njia zitakazotumiwa ni kuongeza ushuru kwa muda.
Rais Rafael Correa amesema tetemeko hilo la kwanza lilisababisha uharibifu wa dola bilioni tatu za Kimarekani.
source: BBC

No comments

+255716829257