Habari mpya

Muhtasari: Habari kuu leo Ijumaa

1. Obama aisihi Uingereza isijitoe EU

ObamaImage copyrightGetty
Image captionObama atazuru Uingereza leo na kukutana na Malkia Elizabeth
Rais wa Marekani Barack Obama amesema anaunga mkono Uingereza kusalia kwenye Muungano wa Ulaya (EU) kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni ya mwezi June.
Bw Obama anaanza ziara yake Uingereza leo. Katika taarifa iloyoandikwa na gazeti la Daily Telegraph, Obama alisema kuwa ikiwa uingereza itaondoka kwenye Muungano wa Ulaya, itakuwa na kazi ngumu ya kupambana na ugaidi, kupata suluhu kwa matatizo ya uhamiaji na uchumi.
Rais Obama anatarajiwa kukutana waziri mkuu wa Uingereza David Cameron kabla ya yeye na mkewe Michelle kushiriki chakula cha mchana na Malkia Elizabeth siku moja baada ya kusherehekea miaka 90.

2. WADA yafuta kibali cha shirika la Uchina

WadaImage copyrightEPA
Image captionWada imesema shirika hilo halikutimiza viwango vinavyohitajika kimataifa
Shirika la kupambana na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu za mwilini WADA limefuta kibali cha shirika la kupambana na matumizi ya madawa hayo nchini China kwa kipindi cha miezi minne baada ya kushindwa kufikia viwango vya kimataifa.
Marufuku hiyo inaamaanisha kuwa shirika hilo la China haliwezi kushiriki katika shughuli zinazoihusu WADA ikiwemo kupima sampuli za damu. Mapema mwezi huu WADA pia ilifuta kibali cha maabara ya shirika la kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza nguvu za mwilini la Urusi.

3. Mjumbe wa UN aeleza shaka kuhusu mazungumzo Syria

WaasiImage copyrightAFP
Image captionWaasi walijiondoa kutoka kwenye mazungumzo wakilalamikia kuendelea kwa mashambulio
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria anasema kuwa hana uhakika ikiwa mazungumzo ya amani yataendelea wiki ijayo.
Staffan De Mistura amezitaka pande zote kuafikiana upya makubaliano ya kisitisha vita na kuruhusu kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu. Wawakilishi wa upinzani nchini Syria walikuwa wameondoka kwenye mazungumzo ya Geneva kupinga mashambulizi ya angani yanayoendelea kufanywa na serikali.
Msafara mkubwa unaosafirisha msaada uliwasili nchini Syria jana katika mji unaozingirwa wa Rastan.

4. Amnesty yasema ina ushahidi dhidi ya Nigeria

ShiaImage copyrightAFP
Image captionWatu zaidi ya 300 waliuawa baada ya jeshi kushambulia watu wa madhehebu ya Shia
Shirika la kupigania haki za binadamu la Amnesty International linasema kuwa lina ushahidi mpya kuhusu kile linachokitaja kuwa mauaji ya watu wengi yaliyofanywa na jeshi la Nigeria mwaka uliopita katika mji ulio kaskazini mwa nchi wa Zaria.
Amnesty inasema kuwa walioshuhudia shambulio hilo dhidi ya watu wa madhehebu ya Shia wameeleza kuwa jeshi lilichoma watu wakiwa hai na kuwapiga risasi watoto wa shule.
Pia Amnesty na afisa mmoja wa serikali eneo hilo walisema kuwa zaidi ya watu 300 waliuawa.

5. Idriss Deby ashinda uchaguzi Chad

DebyImage copyright
Image captionDeby amekuwa madarakani tangu 1990
Rais wa Chad Idriss Deby ameshinda muhula wa tano baada ya kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 50 ya kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais.
Amekuwa madarakani tangu mwaka 1990 kupitia mapinduzi ya kijeshi. Kiongozi wa upinzani Saleh Kebzabo alimaliza wa pili akipata chini ya asilimia 13 ya kura.
Chad ndipo ilipo kambi ya jeshi la nchi tano zinazopambana na kundi la wapiganaji wa Kiislamu kutoka Nigeria la Boko Haram.

6. Viongozi wamuomboleza mwanamuziki Prince

PrinceImage copyrightAFP
Image captionPrince alikuwa maarufu miaka ya 70 na 80
Rambirambi zimekuwa zikitumwa kwa mwanamuziki mmrekani Prince ambaye aliaga dunia siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 57.
Rais Obama alimtaja kuwa mcheza vyombo stadi na mwanamuziki hodari. Mashabiki wamekuwa wakikusanyika nyumbani kwake huko Minneapolis kutoa heshima zao.
Alikuwa maarufu miaka ya 70 na 80. Alitambuliwa kuwa mtunzaji bora zaidi wa nyimbo enzi zake akiuza zaidi ya rekodi milioni 100.

No comments

+255716829257