Habari mpya

'Siri' ya kuonekana kijana katika jeni

Image copyright
Image captionMabadiliko yapo katika jeni MC1R
Wanasayansi w<span >amegundua sehemu ya kwanza ya chembe chembe za DNA ya binaadamu - ambayo inaonekana kuwa siri kuu- inayoathiri vipi watu waze wanavyoonekana.
Mabadiliko yapo katika jeni zinazohusika na kuulinda mwili dhidi ya miale ya jua.
Lakini jeni hizo pia husababisha nywele kugeuka nyekundu na wataalamu wanaonya kwamba huedna mtu akachanganyikiwa na ugunduzi huo kwarangi ya macho, ngozi na hata pia nywele.
Utafiti huo uliopewa jina 'umri unaokadiriwa' umeeandaliwa na chuo kikuu cha Erasmus University Medical Centre Uholanzi pamoja na kampuni ya Unilever.
Dr David Gunn, mwanasayansi mkuu katika kampuni hiyo, anasema ni kitu kisicho cha kawaida ambacho kinafanahamika na wengi.
Ameiambia BBC: "unakutana na watu wawili ambao hujawaona miaka 10 na unaona kwamba mmoja wao hajazeeka zaidi ya vile unavyomkumbuka, na mwingine unaona na kufikiria, 'Heh amefanyika nini?'."
Umri gani?
Picha za watu 2693 ambao hawakujipodoa zilikaguliwa kuona iwapo watatambulika umri wao. Alafu ikalinganishwa na umri wao halisi.
Awamu nyingine ya utafiti nikukagua chembe che,be za DNA kati ya watu hao 2693 kuona kama kuna tofauti yoyote au ulinganisho na wale walioonekana kuwa vijana zaidi ya walivyo.
Image copyrightScience Photo Library
Image captionJeni MC1R inadhihirisha tofuati ya umri
Ushahidi huo ulielekeza kwa jeni ya MC1R - ambayo ni muhimu kwa kutengeneza rangi ya ngozi mwilini na kulinda mwili dhidi ya miale ya sumu kutoka kwa jua.
Lakini jeni hizi zipo katika aina mbalimbali nyingi zinazosababisha nywele kuwa nyekundu.
Utafiti umedhihirisha jeni hiyo ndio inayosababisha watu kuonekana takriban miaka kama miwili chini ya umri wao zaidi ya walio na aina nyengine ya jeni hiyo MC1R.
Hatahivyo watafiti hawawezi kueleza ni kwanini jeni hiyo ina athari hiyo,- walijaribukufanya utafiti kuona iwapo inaweza kubadili ngozi iliyoathirika na miale ya jua lakini haikuonekana kuweza kufanya mabadiliko hayo.
Akizungumzia utafitihuo, Prof Tim Frayling, kutoka chuo kikuu cha Exeter, amesema: "huu ni ugunduzi muhimu unaoonyesha jinsi jeni mwilini zinavyoweza kuathiri ukuwaji wa ugonjwa ndani ya binaadamu.
"Hatahivyo, wachapishajiutafiti huu wamekiri kwamba wanahitaji kufanya uchunguzi zaidi wa namna jeni hizo zinavyofanya kazi ili kuona kama kuna nafasi yoyote ya kutambua muonekano wa mtu kwa kutumia chembe chembe za DNA pekee."
source: BBC

No comments

+255716829257