Habari mpya

Je, ni wakati gani mtoto huwa mtu mzima?

Image captionMahakama nchini Kenya
Jaji mmoja nchini Kenya amemwachilia huru mshukiwa mmoja ambaye alikuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 20 jela kwa kumbaka mtoto wa miaka 13.
Ijapokuwa umri wa mtoto kuwa mtu mzima nchini Kenya ni miaka 18 jaji aliamuru kwamba kesi hiyo haiwezi kuwa ya ubakaji kwa kuwa mtoto huyo alijifanya kuwa mtu mzima na kwamba alikuwa akifurahia kufanya tendo la ngono na wanaume.
Hatahivyo afisi ya mwendesha mashtaka nchini imesema itakata rufaa dhidi uamuzi wa jaji huyo.i.
Naibu mkurugenzi wa mashtaka DPP Vincent Monda amesema kuwa hakufurahishwa na uamuzi wa jaji Said Chitembwe katika mahakama ya rufaa kumwachilia bw Martin Charo.
Jaji Chitembwe alisema kuwa msichana huyo alijifanya kama mtu mzima na hivyobasi mshukiwa hakuwa na makosa.
''Ni kweli kwamba chini sheria ya unyanyasaji wa kingono,mtoto chini ya umri wa miaka 18 hawezi kutoa rukhsa''.
''Hatahivyo iwapo mtoto huyo atajifanya kuwa mtu mzima na kuingia katika nyumba ya mwanamume kwa lengo la kufanya mapenzi,mahakama inafaa kumchukulia mtoto huyo kuwa mtu mzima'',jaji huyo aliamuru wiki iliopita.
''Mshtakiwa hakutarajiwa kuuliza miaka ya mlalamishi kutoka kwa mtu mwengine,uhusiano huo uliendelea hadi kufikia kiwango ambacho umri haukuwa swala muhimu'',alisema jaji huyo akiongezea kwamba ''ni makosa kumpatia kifungo cha miaka 20 bwana Charo ilihali mlalamishi aliupendelea uhusiano wao''.
Jaji huyo baadaye alisema kuwa ''ijapokuwa umma utakasirishwa utakaposikia mtu mzima akijihusisha kimapenzi na mtoto,isisahaulike kwamba mambo yamebadilika na kwamba watoto wadogo sasa wanashiriki katika ngono wakiwa katika umri mdogo''.
Je maoni yako ni yapi,na ni umri gani katika eneo lako ambalo mtoto hutambulika kuwa mtu mzima?

No comments

+255716829257