Habari mpya

Mwanasiasa wa upinzani auawa Nairobi

Image captionMukabana akibebwa na vijana
Mwanasiasa wa upinzani ameuawa kwa kupigwa risasi nje ya nyumba yake katika mji mkuu wa Kenya Nairobi.
Stephene Mukabana ambaye kiongozi wa vijana wa chama cham Orange Democratic Movement (ODM), aliuawa usiku wa jana wakati alienda kumsaidia mtu mmoja aliyekuwa akiporwa na kundi la watu sita kwa mujubu wa gazeti la Standard nchini humo.
Pia gazeti la Standard lilimnukuu gavana wa Nairobi Evans Kidero akisema kuwa kundi la wauaji limfuata na kumuua mwanasiasa huyo wa umri wa miaka 42.
BBC swahili.

No comments

+255716829257