Habari mpya

Meneja: Nyota wa filamu za ngono alikunywa dawa nying

Image copyrightAP
Image captionChyna
Meneja wa aliyekuwa nyota wa filamu za ngono na mwanamiereka Chyna anasema kwamba huenda nyota huyo alifariki kwa kunywa dawa za kulala kupita kipimo chake pamoja na dawa za kupunguza maumivu.
Mwanamiereka huyo alipatikana amefariki nyumbani kwake wiki iliopita.
Meneja wake Anthony Anzaldo,anaamini kwamba kifo chake kilitokana na kunywa dawa kupita kipimo chake.
Hakuna sababu ya kifo chake iliotolewa na afisi ya kaunti ya Los Angeles kwa sababu matokeo ya ukaguzi wa iwapo alikunywa sumu bado hayajatolewa.
''Nadhani alitumia vibaya dawa zake.Anasema kuwa huenda ubongo wake ulijaa mambo mengi na kwamba kulikuwa na mambo mengi ya hisia aliyokuwa nayo moyoni''.
Image captionChyna na mpenziwe
''Lakini hakuwa na huzuni ,ni kwamba alikuwa na mambo mengi kichwani ya kuangazia''.
Anthony anashuku kwamba Chyna alikuwa akijilisha madawa zaidi ya ilivyohitajika
Anasema alikuwa ameanza kumtembelea daktari anayetibu magonjwa ya akili na alikuwa akishiriki katika makundi ya wanawake walio na migogoro majumbani.
source: BBC

No comments

+255716829257