Mbwa atembea kilomita 386 kurejea kwao
Mbwa mmoja amewashangaza watu kwa kutembea kilomita 386 kurejea alikozaliwa kutoka Cumbria Uingereza.
Jibwa hilo lililokuwa linaishi Cockermouth Ceredigion lilitoroka tarehe 8 Aprili na kurejea Cumbria alikozaliwa nyumbani kwa Alan na Shan James.
Mmiliki wake hajui jibwa hilo lilifikaje huko.
Pero, anayesemekana kuwa na umri wa miaka 4 ni mweledi wa kuchunga kondoo hata hivyo haijulikani aliwezaje kusafiri umbali huo wote bila msaada wa mtu.
Mkewe James, anayeishi na wanawe watano huko Penrhyncoch anasema kuwa jumatano iliyopita mumewe alitoka nje jioni akitaka kupeleleza kwanini kondoo wake walikuwa wakipiga makelele usiku.
Ghafla akamuona Pero.
Jibwa hilo lilianza kurukaruka kumfurahia mumewe Alan na kumwacha amepigwa na butwaa.
"hakuna aliyetujulisha kuwa atamrejesha mbwa huyo wala hakuna aliyetuuliza hadi wa leo iwapo amerudi nyumbani licha ya kuwa yuko na kifaa cha kutambua aliko''
''Tunajua kuwa mbwa anaweza kurejea nyumbani lakini umbali wa zaidi ya kilomita 380 ni maajabiu haya''
''Ajabu ni kuwa aliporejea nyumbani alikuwa ameshiba.''
Hakutaka kula na kuibua dhana kuwa huenda alikuwa analishwa na mtu ambaye hadi sasa hawamjui ni nani.
source: BBC
No comments
+255716829257