Habari mpya

Julius Malema atekwa na kuachiwa na polisi

Image captionJulius Malema
Maafisa wa polisi Afrika Kusini walimvizia kiongozi wa chama cha upinzani cha Economic Freedom Fighters (EFF) Julius Malema katika barabara moja ya Johannesburg jana usiku katika tukio ambalo kiongozi huyo anadai linalenga kumtishia ili alegeze kamba dhidi ya rais Jacob Zuma.
Kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter cham chake cha EFF kinasema kuwa
''Kamanda wetu aliviziwa na takriban magari kumi ya polisi ambao wote walimelekezea mtutu wa bunduki baada ya kulizuia gari lake katika makutano ya barabara ya Grayston .
''Cha ajabu ni kuwa hakukuwa na gari lolote ila yale ya polisi.''
''Kamanda wetu (Malema) alipotoka nje hakuna aliyefyatua risasi.''
''Ila walirejea ndani ya magari yao na kuondoka kwa haraka pahala hapo.''
Image copyright
Image captionEFF na bwana Malema wanaongoza kampeini ya kumng'oa rais Zuma madarakani kufuatia utepetevu na ubadhirifu wa mali ya umma.
''Hii inaonesha wazi kuwa serikali ambayo sasa imekabwa koo na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na ubadhirifu wa mali ya umma imeanza kutumia mbinu chafu na nguvu kinyume cha sheria.''
Msemaji wa polisi alisema kuwa hakufahamu lolote kuhusu tukio hilo.
EFF na bwana Malema wanaongoza kampeini ya kumng'oa rais Zuma madarakani kufuatia utepetevu na ubadhirifu wa mali ya umma.
Chama hicho kilipata uungwaji mkono juma lililopita mahakama ya juu zaidi nchini humo ilipompata Zuma na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka yake na ubadhirifu wa fedha kuhusiana na ukarabati wa makazi yake ya Nkandla.
Zuma akekanusha kufanya makosa yeyote ila amekubali kurejesha fedha zilizotumika katika ukarabati huo ilokiuka sheria za nchi.

No comments

+255716829257