Habari mpya

Mambo 5 muhimu kuhusu Jumanne Kuu

Clinton TrumpImage copyrightAFP y Reuters
Image captionClinton anaongoza kwa wajumbe kwa sasa upande wa Democratic naye Trump upande wa Republican
Siku ya leo huwa siku muhimu sana katika shughuli ya kuwateua wagombea urais wa vyama vya Republican na Democratic na ndio maana hujulikana kama Jumanne Kuu.
Huwa ni siku ambayo wagombea hudhihirisha ubabe wao na wengine kuishiwa na nguvu.
Majimbo 12 hufanya mchujo siku hii.

1. Mbona kufanya mchujo majimbo mengi?

Jumanne Kuu ilianzishwa 1988 kujaribu kutoa taswira kamili ya msimamo wa Wamarekani kuhusu wagombea na uwezo wao. Ilibainika kwamba jimbo la Iowa, ambalo huwa la kwanza kufanya mchujo ni ndogo na wagombea hufanya kampeni sana huko. Wagombea wadogo wasio na rasilimali, kama vile Rick Santorum mwaka 2012, hufanya vyema sana huko. Jumanne Kuu hukusudiwa kuwaweka wagombea kwenye changamoto na gharama ya kufanya kampeni ya kitaifa.

2. Ni majimbo mangapi yanafanya mchujo?

Katika chama cha Republican: Majimbo kumi na moja yatafanya kura ya mchujo. Alabama, Arkansas, Georgia, Massachusetts, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont, Virginia, Alaska na Minnesota.
Katika chama cha Democratic: Kuna majimbo kumi na moja yanayofanya mchujo. Alabama, Arkansas, Georgia, Massachusetts, Oklahoma, Tennessee, Texas, Vermont, Virginia, Colorado na Minnesota. Jimbo la American Samoa pia hufanya mchujo huku wanachama wa Democratic walio ng’ambo nao pia wakituma kura zao.
Shughuli nyingine: Maafisa wa chama cha Republican wataandaa hafla zinazohusiana na mchujo Colorado, North Dakota na Wyoming pamoja na maeneo ya American Samoa na Guam, lakini hakutapigwa kura zozote. Viongozi wa vyama katika majimbo hayo hatimaye watawatengea wagombea wajumbe wakitilia maanani mchango wa wanachama.

3. Matokeo yanatarajiwa lini?

Upigaji kura utamalizika 1900 au 2000 EST (saa sita usiku au 01:00 GMT Jumatano) na matokeo yatatarajiwa kuanzia wakati huo.
Katika jimbo la Alaska, upigaji kura huendelea hadi saa sita usiku EST (05:00 GMT).
Utafiti wa kura unaofanywa baada ya watu kupiga kura hutoa vidokezo vya nani atashinda.
Ni wajumbe wangapi wanashindaniwa?
  • Republican: Kuna wajumbe 595 wa kushindaniwa, ambao ni 25% ya wajumbe wote. Mgombea wa Republican anahitaji wajumbe 1,237 kushinda uteuzi.
  • Democratic: Hillary Clinton na Bernie Sanders watashindania wajumbe 865. Mgombea wa Democratic anahitaji wagombea 2,383.
Wagombea na wajumbe waliopata
MgombeaAlio naoAnaowahitaji
Democratic
Clinton5461,837
Sanders872,296
Republican
Trump821,155
Cruz171,220
Rubio161,221

4. Ni majimbo yapi muhimu?

Texas: Jimbo hili ni kubwa na muhimu. Lina idadi kubwa ya wajumbe (55 Republican, 252 Democratic). Aidha, ndiko anakotoka Seneta Ted Cruz. Iwapo atashindwa na Trump kwake nyumbani, litakuwa pigo kuu.
Massachusetts: Wapiga kura wa msimamo wa wastani wanaweza kupunguza kasi ya Bw Trump. Mchujo wa Massachusetts ni wazi, maana kwamba yeyote anaweza kushiriki bila kuzingatia chama.

5. Jumanne Kuu itakuwa mwisho wa safari kwa yeyote?

Awali, Jumanne Kuu imekuwa muhimu sana. Mitt Romney alihakikishiwa uteuzi wake baada ya kushinda Jumanne Kuu 2012. Mwaka huu mambo si wazi sana. Wagombea kama vile Marco Rubio na John Kasich huenda wakasubiri hadi 15 Machi mchujo wa majimbo makubwa kama vile Florida na Ohio. Ben Carson hata hivyo amedokeza huenda akahitimisha kampeni yake Jumanne Kuu baada yake kutofanya vyema.
CarsonImage copyrightAP
Image captionBen Carson hajafanya vyema kufikia sasa
Upande wa Democratic, Bw Sanders, mpinzani pekee wa Bi Clinton, anatarajiwa kuendelea na kampeni yake.

No comments

+255716829257