Habari mpya

Polisi walioua msichana Kenya wafungwa miaka saba

wakili
Image captionWakili wa Veronica Gitahi na Issa Mzee amesema atakata rufaa
Maafisa wawili wa polisi waliopatikana na hatia kuhusiana na mauaji ya msichana wa umri wa miaka 14 nchini Kenya wamefukumiwa kifungo cha miaka saba jela kila mmoja.
Maafisa hao Veronica Gitahi, aliyekuwa afisa wa uchunguzi wa jinai wa cheo cha inspekta na konstebo Issa Mzee wamehukumiwa baada ya kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia wiki iliyopita.
Jaji alikataa tetesi zao kwamba walifyatua risasi wakijilinda baada ya kushambuliwa na msichana huyo Kwekwe Mwandaza Agosti 2014 katika eneo la Kinango, Kwale eneo la Pwani ya Kenya.
Aliuawa wakati wa operesheni ya kumsaka mhalifu.
Familia ya Kwekwe haijaridhishwa na uamuzi huo na mamake amezimia muda mfupi baada ya hukumu kutolewa. Amekimbizwa hospitalini.
Image captionMamake Kwekwe amepelekwa hospitalini
Maafisa wa mashirika ya kutetea haki za kibinadamu wamesema hukumu hiyo haitoshi.
Khelef Khalifa, mkurugenzi mkuu wa shirika la Muslims for Human Rights (Muhuri) amesema maafisa hao walifaa kufungwa jela kati ya miaka 15 na maisha.
Francis Auma, afisa katika shirika la Haki Africa, amesema kutolewa kwa hukumu hiyo kutatoa ujumbe mkal kwa maafisa wa polisi.
Upande wa washtakiwa umeomba waachiliwe huru kwa dhamana wakijiandaa kukata rufaa. Uamuzi kuhusu ombi lao utatolewa baadaye leo.

No comments

+255716829257