Habari mpya

MJANE WA KIONGOZI WA KUNDI LA"IS" ASHTAKIWA KWA MAUAJI.


Image copyrightThe Daily Courier
Image captionKayla Mueller

Mjane wa mmoja wa viongozi wakuu wa zamani wa kundi la Islamic state ameshtakiwa na njama za kifo cha mateka mmoja wa Marekani,mamlaka ya Marekani imesema.
Kayla Mueller alitekwa nyara wakati alipokuwa akifanya kazi katika mji wa Aleppo,nchini Syria na kufariki mwaka uliopita.
Mwanamke huyo aliyeshtakiwa, Nisreen Assad Ibrahim Bahar,anayejulikana kama Umm Sayyaf kwa sasa anazuiliwa nchini Iraq.
Waendesha mashtaka wanasema Sayyaf alimzuia Mueller,na kuruhusu abakwe na kiongozi wa IS Abu Bakr al-Baghdadi.
  • Je, Kayla Mueller alikuwa nani?
Mumewe Nisreen,Abu Sayyaf,ameelezewa kuwa waziri wa mafuta na gesi wa Islamic State na huripoti moja kwa moja kwake Baghdadi.
Abu Sayyaf alifariki mwezi Mei wakati alipovamiwa nyumbani kwake na vikosi maalum vya Marekani.
Mkewe baadaye alikabidhiwa mamlaka ya Iraq ili ashtakiwe.
Taarifa ya idara ya haki nchini Marekani,inasema kuwa iliunga mkono kushtakiwa kwake,lakini itaendelea kutafuta haki ya Kayla.
''Hatutasita katika juhudi zetu,za kuwatambua,kuwatafuta na kuwakamata wale wanaotekeleza utekaji nyara na mauaji ya raia wa Marekani,''alisema naibu mkurugenzi Paul Abbate.

No comments

+255716829257