KESI YA ZUMA KUSIKILIZWA NA MAHAKAMA KUU NCHINI AFRIKA KUSINI.
Mahakama ya katiba nchini Afrika Kusini hivi sasa inasikiliza kesi ya kuhusu ikiwa rais Jacob Zuma anapaswa kulipa mamilioni ya dola pesa za walipa kodi zilizotumiwa kukarabati nyumba yake binafsi.
Vyama viwili vya upinzani vimeomba pia uamuzi uchukuliwe kuhusu uhuru wa ulinzi wa mali ya umma, baada ya ripoti zao kuhusiana na hilo kupuuzwa na bunge.
Ingawa wiki iliyopita rais Zuma alitangaza kuwa yuko tayari kulipa mchango wake , hilo linaonelewa na wapinzani wake wa kisiasa kama juhudi ndogo zilizochelewa.
Zaidi ya dola milioni 23 zilitumiwa katika kuboresha makazi ya Bwana Zuma, kikiwemo kidimbwi cha kuogelea, zizi la mifugo, kituo cha tamasha, kwa kutumia pesa za mlipa kodi katika sakata inayoangaliwa na wengi kama aibu ya taifa.
Tume huru ya uchunguzi, mwaka 2014 ilibaini kuwa Bw Zuma alijinufaisha kwa pesa za umma na kwamba anapaswa kulipa pesa pesa alizotumia, lakini madai hayo yalipuuzwa hadi wiki iliyopita.
Licha ya kwamba rais mwenyewe alitakaswa dhidi na polisi kwamba hakufanya kosa lolote, kesi hii mbele ya mahakama ya katiba ni zaidi kuhusu kazio ya bunge ya kuwajibisha serikali.
kutoka:BBC Swahili.
No comments
+255716829257