KOREA KASKAZINI YAFTATUA KOMBORA, JE IMEKAIDI AGIZO LA UMOJA WA MATAIFA??
Korea Kaskazini imerusha kombora la masafa marefu anga ya mbali kinyume na maazimio ya umoja wa mataifa na kusababisha shutuma za kimataifa.
Vyombo vya habari nchini Korea Kusini vinasema kuwa kombora hili lilipitia anga ya Japan katika kisiwa cha Okinawa.
Tangazo kupitia kwa runinga ya taifa ya Korea Kaskazini lilisema kuwa jaribio hilo lilifanikiwa kuweka mtambo wake wa satellite katika sayari ya mbali.
Naye waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa marekani John Kerry amesema kuwa uzinduzi huo hauhatarishi tu usalama wa rasi ya Korea bali pia eneo lote pamoja na Marekani.
Licha ya kuwa Korea Kaskazini inasema kuwa nia yake ilikuwa ni kupeleka chombo cha angani katika sayari ya mbali , wakosoaji wake wanaamini kuwa Korea inaunga zana za kinyukilia zenye uwezo wa kufika nchini Marekani.
Rais wa Korea Kusini Park Geun-hye amesema kuwa kitendo hicho ni cha uchokozi na kutaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya Korea Kaskazini.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ametaja jaribio hilo kama kitendo ambacho hakiwezi kuvumiliwa na kuongeza kuwa huo ni ukiukaji wa azimio la umoja wa mataifa.
Mshirika mkuu wa Korea Kaskazini China pia wamejutia kuhusu uzinduzi huo wa Korea Kaskazini ikidai kuwa imefanikiwa kupeleka satellite anga ya juu.
Ripoti zinasema kuwa Marekani, Japan na Korea Kusini zimeomba kufanyika kwa mkutano wa dharura wa baraza la usalama la umoja wa mataifa leo Jumapili.
Wakosoaji wake hata hivyio wanasema kuwa ni jaribio la teknolojia ya makombora iliyopigwa marufuku.
Vyombo vya habari nchini Korea Kusini vinasema kuwa kombora hilo lilifyatuliwa kutoka katika kituo cha makombora Kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Korea Kaskazini inasema kuwa nia yake ilikuwa ni kupeleka chombo cha angani katika sayari ya mbali , lakini wadadisi wanaamini kuwa Korea inaunga zana za kinyukilia zenye uwezo wa kufika nchini Marekani.
Marekani , Japan na Korea Kusini wameitisha mkutano wa dharura wa baraza la ulinzi la umoja wa mataifa leo Jumapili.
No comments
+255716829257