Habari mpya

JE UNAJUA KUWA TEKNOLOJIA INAKUA KILA SIKU..?? SOMA UJIONEE UBUNIFU WA HALI YA JUU.

Teknolojia hubadilika mara kwa mara na kila siku kuna mambo mapya yanayovumbuliwa na mitindo pia kubadilika.
Hapa, kuna makala tano kuhusu teknolojia ambazo hazifai kukupita.

1. Li-fi ina kasi mara 100 zaidi ya Wi-fi

Teknolojia mpya ya kutuma data ijulikanayo kama Li-fi imefanyiwa majaribio.
Li-fi ina uwezo wa kumfanya mtumiaji kupata huduma ya mtandao mara 100 zaidi ya Wi-Fi na hutoa kasi ya hadi Gigabait moja kwa kila sekunde. Soma zaidi hapa:Li-fi ina kasi mara 100 zaidi ya Wi-fi
Image copyrightTHINKSTOCK

2. Choo kinachojifungua na kujiosha

Choo cha kisasa ambacho kina uwezo wa kujifungua unapokaribia na pia kujiosha, ni moja ya vitu vinavyoonyeshwa katika maonyesho ya kimataifa ya teknolojia mpya za bidhaa za elektroniki Las Vegas.
Choo hicho, kilichopewa jina Neorest, pia humsafisha anayekitumia kwa kifaa kinachotoa maji moto na hewa mtu akiwa ameketi. Soma zaidi hapa: Choo kinachojifungua na kujiosha
Image copyrightToto

3. Mercedes yazindua lori linalojiendesha

Mwanzo ilikuwa ni magari madogo sasa kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari Daimler Mercedes-Benz imezindua lori linalojiendesha lenyewe!
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo yenye asili yake nchini Ujerumani,Wolfgang Bernhard alibofya kidude na mara lori likachukua usukani na kuenda lenyewe pasi na kusababisha ajali ya aina yeyote. Soma zaidi hapa: Mercedes yazindua lori linalojiendesha

4. Je una simu ya Android? Soma utafiti huu

Simu za kisasa zinazotumia mfumo wa Android zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi sana.
Uchunguzi umebaini kuwa simu zinazotumia mfumo huo zinaweza kufuatiliwa kwa urahisi mno pasi na kutumia kifaa cha GPS yake. Soma zaidi: Je una simu ya Android?
Image copyrightGetty

5. Samsung yakiri TV zake zinanasa sauti

Samsung imewaonya wateja wake kuhusu kutojadili mambo yao ya kibinafsi mbele ya televisheni zao.
Onyo hilo ni kwa wale watazamaji ambao hudhibiti televisheni zao kwa kutumia sauti.
Baadhi ya runinga hizo za kisasa husikiliza mambo ambayo wanasema na zinaweza kuwasilisha ujumbe kwa Samsung au mashirika yanayohusiana na Samsung kibiashara. Soma zaidi hapa: Samsung yakiri TV zake zinanasa sauti

No comments

+255716829257