Habari mpya

JE RWANDA INAPANGA KUMPINDUA NKURURUNZINZA??

Image copyrightAP
Image captionBaraza la Usalama la UN
Ripoti ya siri katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa inaishtumu Rwanda kwa kuwasajili na kuwapa mafunzo wakimbizi wa Burundi kwa lengo la kumpindua rais wa Burundi Pierre Nkurunziza.
Kulingana na chombo cha habari cha Reuters,ripoti hiyo ya wataalam wa Umoja wa Mataifa ambao hufuatilia vikwazo dhidi ya taifa la DR Congo inadai kwamba mafunzo yalifanywa katika kambi moja ya msituni nchini Rwanda,kwa mujibu wa Reuters.
Wataalam hao wamesema katika ripoti hiyo kwamba walizungumza na wapiganaji 18 wa Burundi mashariki mwa mkoa wa kusini wa Kivu nchini DRC,kulingana na chombo hicho cha habari.
''Wote waliliambia kundi hilo kwamba wamesajiliwa katika kambi ya wakimbizi ya Mahama mashariki mwa Rwanda mnamo mwezi Mei na Juni mwaka 2015 na walipatiwa miezi miwili ya mafunzo ya kijeshi na walimu wao,ambao walishirikisha wanajeshi wa Rwanda'',Reuters imenukuu ripoti hiyo ikisema.
Rwanda haijatoa tamko lolote kuhusu ripoti hiyo iliofichuliwa,lakini imekana madai kama hayo hapo awali.
Image copyrightReuters
Image captionGhasia za Burundi
Burundi imekabiliwa na machafuko tangu mwezi Aprili,wakati rais Pierre Nkurunziza alipotangaza kwamba atawania muhula wa tatu wa urais,ambao alishinda.
Alinusurika jaribio la mapinduzi mnamo mwezi Mei,na majenerali wake wanne wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kupanga kumpindua

No comments

+255716829257