Habari mpya

SENTENSI CHACHE ZA WAZIRI MKUU MSTAFU MH. FREDRICK SUMAYE BAADA YA KUTEMBELEWA GAFLA HOSPITALINI NA RAISI MAGUFULI.


Kumekuwa na ripoti mfululizo kwenye vyombo vya habari kuhusu kuumwa na kulazwa kwa Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye katika hospitali ya Muhimbili huku kukiwa hakuna ripoti inayotaarifu ugonjwa wake.
Hii haikuwa ziara ya ghafla, ilikuwa msafara wa Rais Magufuli katika hospitali ya Muhimbili kwenda kumjulia hali mzee Sumaye japokuwa hata yeye mwenyewe hakuwa na taarifa ya ujio wa ugeni wa Rais >> ‘Nimeshukuru sana Rais kuja kunitembelea hapa ni jambo kubwa, nimeshtuka kwa sababu sikutegemeana sikupata taarifa yoyote…. namshukuru Rais Magufuli kwa upendo wake, anaonesha kujali sana watu wake.‘<<-Frederick Sumaye.
AM POMBE
Hapo ni Rais Magufuli, Mzee Sumaye pamoja na mke wake, Mama Esther Sumaye.
Sentensi zake nyingine hizi hapa >> ‘Naendelea vizuri, hali yangu ni nzuri natumaini baada ya muda mfupi nitatoka hospitali‘<<- Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye.
source: millardayo.com..http://millardayo.com/jpm1101/

No comments

+255716829257