Habari mpya

RAIS MAGUFULI AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA VITAMBULISHO.

MagufuliImage copyrightAFP
Image captionRais Magufuli anataka uchunguzi ufanywe kuhusu matumizi ya Sh.179.6 bilioni
Rais wa Tanzania John Magufuli, ametengua uteuzi wa mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kupisha uchunguzi katika mamlaka hiyo.
Taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imesema kando na kumsimamisha kazi Bw Dickson Maimu, Rais Magufuli ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.
“Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Sh179.6 bilioni. Kiasi hiki ni kikubwa na Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizi zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa,” imesema taarifa kutoka kwa Bw Sefue.
Kadhalika, Rais amewasimamisha kazi Bw Joseph Makani (Mkurugenzi wa TEHAMA), Bi Rahel Mapande (Afisa Ugavi Mkuu), Bi Sabrina Nyoni (Mkurugenzi wa Sheria) na Bw George Ntalima (Afisa usafirishaji).
Rais, aidha, ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na mamlaka hiyo.
Kadhalika, ameelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalum wa hesabu za mamlaka hiyo, ikiwemo ukaguzi wa “kupokea thamani kwa pesa zilizolipwa” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa.
Kwingineko, katika Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa, Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Juma Maalim ameteuliwa balozi wa Tanzania nchini Kuwait.
Mabalozi Bi Batilda Salha Buriani, aliyeko Tokyo, Japan na Dkt. James Alex Msekela, aliyeko Rome, Italia, hata hivyo wameagizwa kurejea nyumbani baada ya kumaliza muda wao wa kuhudumu
Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza Bw Peter Allan Kallaghe naye amerejeshwa katika Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.

No comments

+255716829257